Apr 03, 2023 09:52 UTC
  • Madaktari Kenya watahadharisha kuhusu aina mpya za magonjwa ya zinaa

Madaktari wamewataka Wakenya kuwa na tahadhari baada ya kugunduliwa aina mbili mpya za magonjwa ya zinaa (STIs).

Wanasayansi katika Taasisi ya Utafiti wa Matibabu ya Kenya (Kemri) wamepata mabadiliko mawili mapya ambayo wanasema hayajawahi kuonekana katika jeni zinazohusiana na kisonono na klamidia.

Ugunduzi huo umetangazwa huku wachunguzi wakitaka kuelewa ni kwa nini hospitali mbili katika Kaunti ya Busia, ambayo inapakana na Uganda, zilikuwa zikirekodi visa vya magonjwa ya zinaa.

Mtandao wa Kenya wa Nation umeandika kuwa Prof Samson Muuo, msaidizi wa mwanasayansi mkuu wa utafiti katika Kituo cha Utafiti wa Mikrobiolojia huko Kemri, ameeleza kwamba wameshangaa kuona kwamba wanawake 424 wa Kenya walio na umri wa miaka 15 na zaidi waliopimwa kutoka hospitali hizo mbili walipatikana na ugonjwa wa kisonono na klamidia.

Watafiti wanasema kwamba hawakupata jeni za kawaida zilizoripotiwa zinazohusiana na mabadiliko yaliyotambuliwa hayakuwa ya asili ya kawaida kutoka kwa yale yaliyoripotiwa hapo awali.

Prof Muuo ameendelea kubainisha kwamba mabadiliko ya kisonono na klamidia waliyopata yalikuwa yakishambulia kwa pamoja.

Tags