Kamanda wa waasi wa LRA akamatwa CAR
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i985-kamanda_wa_waasi_wa_lra_akamatwa_car
Polisi ya Jamhuri ya Afrika ya Kati imetangaza kuwa kamanda wa kundi la waasi kutoka Uganda la Lord's Resistance Army (LRA) aliyetiwa nguvuni nchini humo ametambuliwa kuwa ni Okot Odek ambaye ni miongoni mwa viongozi waandamizi wa genge hilo hatari.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Feb 11, 2016 00:06 UTC
  • Kamanda wa waasi wa LRA akamatwa CAR

Polisi ya Jamhuri ya Afrika ya Kati imetangaza kuwa kamanda wa kundi la waasi kutoka Uganda la Lord's Resistance Army (LRA) aliyetiwa nguvuni nchini humo ametambuliwa kuwa ni Okot Odek ambaye ni miongoni mwa viongozi waandamizi wa genge hilo hatari.

Okot Odek alikamatwa Jumatatu iliyopita na kundi la wanamgambo wa Seleka wakishirikiana na polisi ya Jamhuri ya Afrika ya Kati lakini utambulisho wake ulijukulana jana baada ya kusailiwa. Okot Odek sasa amekabidhiwa kwa askari wa Marekani walioko nchini Uganda. Odek ambaye alikuwa akitumia jina bandia la Kamanda Sam, alikuwa miongoni mwa makanda wa ngazi za juu wa kundi la LRA na mlinzi binafsi wa kiongozi wa kundi hilo, Joseph Kony.

Umoja wa Mataifa unasema kuwa kundi la waasi wa Uganda la Lord's Resistance Army (LRA) limeua zaidi ya watu laki moja na kuteka nyara watoto elfu sitini ambao baadhi yao wanatumiwa kama watumwa wa ngono.

Kamanda mwinginme wa kundi la LRA, Dominic Ongwen, alikamatwa na kundi hilo hilo la Seleka yapata mwaka mmoja uliopita huko CAR na kukabidhiwa kwa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) iliyoko Hague nchini Uholanzi.