UN yarefusha muda wa vikwazo dhidi ya Kongo DR
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i9883-un_yarefusha_muda_wa_vikwazo_dhidi_ya_kongo_dr
Baraza la Usalama la Umoja wa mataifa, umerefusha muda wa vikwazo dhidi Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kwa mwaka mmoja zaidi.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jun 24, 2016 10:33 UTC
  • UN yarefusha muda wa vikwazo dhidi ya Kongo DR

Baraza la Usalama la Umoja wa mataifa, umerefusha muda wa vikwazo dhidi Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kwa mwaka mmoja zaidi.

Baraza hilo lilichukua maamuzi hayo baada ya kupitia azimio la kurefusha vikwazo vya silaha na fedha nchi hiyo, ambavyo vitaendelea hadi tarehe Mosi Julai mwaka 2017. Kadhalika baraza hilo limerefusha muda wa kuendelea na majukumu yake timu ya wataalamu wa Umoja wa Mataifa inayojishughulisha na kusimamia utekelezwaji wa vikwazo hivyo dhidi ya nchi hiyo hadi tarehe Mosi Agosti mwaka kesho 2017. Vikwazo vya silaha dhidi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo vilianza kutekelezwa baada ya wanachama 15 wa baraza hilo kupasisha azimio la kuzuia kuiuzia na kununua silaha Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Hata hivyo Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limesisitiza kuwa, vikwazo hivyo vinawahusu watu au taazizi ambazo zimehusika na machafuko nchini humo. Aidha limezitaka nchi zote zikiwemo za eneo na askari wa kusimamia amani wa Umoja wa Mataifa nchini Kongo DR kushirikiana na wataalamu wa umoja huo katika kusimamia utekelezwaji wa vikwako vilivyotajwa.