Waislamu wa Shia nchini Misri walalamikia mbinyo wa serikali dhidi yao
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i9889-waislamu_wa_shia_nchini_misri_walalamikia_mbinyo_wa_serikali_dhidi_yao
Waislamu wa Shia nchi Misri wamekosoa vikali mashinikizo na mbinyo unaotekelezwa na serikali ya nchi hiyo dhidi yao.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jun 24, 2016 22:15 UTC
  • Waislamu wa Shia nchini Misri walalamikia mbinyo wa serikali dhidi yao

Waislamu wa Shia nchi Misri wamekosoa vikali mashinikizo na mbinyo unaotekelezwa na serikali ya nchi hiyo dhidi yao.

Imad Qindil, kiongozi wa jumuiya ya Waislamu wa Shia nchini humo ameyasema hayo katika mahijiano aliyoyafanyiwa na kituo cha habari cha al-Fajru Libi, ambapo alizungumzia hatua ya kuzuia ujenzi wa Husseiniyyah kwa ajili ya Waislamu hao ndani ya taifa hilo. Qindil amesema kuwa, ni suala la kushangaza ambapo hadi sasa hakuna jengo hata moja la Husseiniyyah lililojengwa nchini Misri licha ya kuwepo sheria ya uhuru wa kuabudu. Mwanaharakati huyo wa Kishia nchini Misri amefafanua kuwa, Mawahabi wa Saudia wanafanya chini juu kuhakikisha wanafuta fikra tofauti na kundi hilo, na kwamba tayari Chuo Kikuu cha Kiislamu cha al-Azhar nchini Misri kimekwishaathiriwa na fikra hizo za Kiwahabi. Imad Qindil pia ameashiria baadhi ya tuhuma bandia zinazotolewa na Mawahabi dhidi ya Waislamu wa Kishia nchini humo na kusisitizia kuwa, ni jambo lililowazi kwamba, maulama wa Shia na katika hauza tofauti wamekuwa wakitoa fatwa za kukemea kuwatusi masahaba au wake wa Mtume (saw) . Amesema kuwa, licha ya ukweli huo, lakini Mawahabi wamekuwa wakiwanasibisha Waislamu hao wa Shia na tuhuma hizo kwa lengo tu la kupotosha ukweli huo. Kadhalika amelaani hatua ya mashinikizo makali dhidi yao na kusema kuwa, Mashia wanaoishi nchini Misri pindi wanapofanya safari nchini Iran au Iraq, basi huwa wanawekewa machinikizo chungu nzima pale wanaporejea nchini humo.