Ulaya: Uchunguzi ufanyike kuhusu mauaji ya umati mashariki mwa Kongo
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i9916-ulaya_uchunguzi_ufanyike_kuhusu_mauaji_ya_umati_mashariki_mwa_kongo
Bunge la Ulaya limetaka kufanyika uchunguzi kuhusu kuuliwa kwa umati raia huko mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jun 25, 2016 01:59 UTC
  • Ulaya: Uchunguzi ufanyike kuhusu mauaji ya umati mashariki mwa Kongo

Bunge la Ulaya limetaka kufanyika uchunguzi kuhusu kuuliwa kwa umati raia huko mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Bunge la Ulaya jana Ijumaa liliitaka serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ifanye uchunguzi kuhusu mauaji ya umati yaliyofanywa dhidi ya raia katika maeneo ya mashariki mwa nchi hiyo ukiwemo mji wa Beni unaopatikana katika mkoa wa Kivu ya Kaskazini.

Watoto na wanawake zaidi ya 1160 waliuliwa kati ya mwezi Oktoba mwaka 2014 hadi mwezi Mei mwaka huu katika maeneo ya Beni, Lubero na Butembo yanayopatikana katika mkoa wa Kivu ya Kaskazini.

Bunge la Ulaya limeyataja mauaji hayo ya umati kuwa ni jinai ya kivita. Bunge hilo pia limeutaka Umoja wa Ulaya kuwawekea vikwazo wale wote waliohusika na mauaji hayo. Bunge hilo pia limeripoti kuwa kutumwa makundi yenye silaha katika vijiji vingi vya maeneo ya Beni na Lubero kumesababisha raia 1470 kukimbia makazi yao kati ya mwezi Oktoba mwaka juzi hadi mwezi Mei mwaka huu.