Jeshi Nigeria laangamiza wanachama 10 wa kundi la Boko
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i9955-jeshi_nigeria_laangamiza_wanachama_10_wa_kundi_la_boko
Wanachama kumi wa kundi la kigaidi la Boko Haram wameuawa kufuatia operesheni ya jeshi la Nigeria katika miji ya Gamboru na Ngala iliyoko katika jimbo la Borno.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jun 25, 2016 11:04 UTC
  • Jeshi Nigeria laangamiza wanachama 10 wa kundi la Boko

Wanachama kumi wa kundi la kigaidi la Boko Haram wameuawa kufuatia operesheni ya jeshi la Nigeria katika miji ya Gamboru na Ngala iliyoko katika jimbo la Borno.

Meja Jenerali Lucky Irabor mmoja wa makamanda waandamizi katika jeshi la Nigeria amewaambia waandishi wa habari mjini Abuja kwamba, wanachama hao kumi wa kundi la Boko Haram wameuawai katika operesheni kabambe ya jeshi ambapo raia saba waliokuwa wakishikiliwa mateka na wanamgambo hao wameokolewa pia kutokana mikononi mwa kundi hilo.

Meja Jenerali Lucky Irabor ameongeza kuwa, silaha na zana nyingi za kijeshi zimekamatwa pia na jeshi la Nigeria katika operesheni yake hiyo.

Miji ya Gamboru na Ngala ambayo inapakana na Cameroon kwa muda mrefu ilikuwa katika udhibiti wa wanamgambo wa Boko Haram ambapo katika kipindi hicho wanamgambo hao mbali na kuvidhibiti kikamilifu vituo vya jeshi na vya usalama walifanya mauaji ya kutisha dhidi ya raia.

Ikumbukwe kuwa, mwezi Machi mwaka huu, Benki ya Dunia ilitangaza kuwa, wanamgambo wa kundi la kigaidi la Boko Haram la nchini Nigeria hadi sasa wameua watu zaidi ya 20 elfu na kusababisha hasara ya dola bilioni 5.9 katika jimbo la Borno. Aidha ripoti hiyo ilisema zaidi ya watu milioni mbili wamefanywa wakimbizi kufuatia ugaidi wa Boko Haram.