Askari wa Kongo DR waharibu ngome ya waasi wa Rwanda
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i9991-askari_wa_kongo_dr_waharibu_ngome_ya_waasi_wa_rwanda
Duru za habari nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, zimearifu kuharibiwa moja ya ngome za waasi wa Rwanda eneo la mashariki mwa nchi hiyo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jun 26, 2016 02:58 UTC
  • Askari wa Kongo DR waharibu ngome ya waasi wa Rwanda

Duru za habari nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, zimearifu kuharibiwa moja ya ngome za waasi wa Rwanda eneo la mashariki mwa nchi hiyo.

Njike Kaiko, msemaji wa operesheni za jeshi la serikali ya nchi hiyo ameyasema hayo katika hafla ya Sokola 2, ambalo ni jina la operesheni hizo na kuongeza kuwa, askari wa nchi hiyo kwa kushirikiana na wale wa kusimamia amani wa Umoja wa Mataifa wamefanikiwa kusambaratisha kabisa moja ya kambi muhimu za waasi wa Rwanda wa FDLR. Kwa mujibu wa Kaiko, operesheni hiyo iliyofanikiwa ilifanywa katika eneo la Rutshuru, lililoko katika mkoa wa Kivu Kaskazini, mashariki mwa nchi hiyo. Katika operesheni hiyo, jeshi la Kongo limedhibiti pia silaha za waasi hao. Aidha msemaji wa operesheni za Sokola 2 nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, amesisitiza azma ya kuendelezwa operesheni hizo katika maeneo ya mashariki mwa nchi hiyo, kwa kushirikiana na askari wa kusimamia amani wa Umoja wa Mataifa.