-
Rais wa Somalia: Tutazuia Israel kuimarisha ushawishi wake Somaliland
Aug 03, 2026 11:10Rais wa Somalia, Hassan Sheikh Mohamud, amesema kwamba Serikali ya Shirikisho itachanganya "nguvu na hekima" ili kuzuia "Israel" kupata nafasi au kuanzisha ushawishi wa kudumu katika eneo la "Somaliland," akisisitiza kwamba Mogadishu ingali inashikamana na umoja wa ardhi na mamlaka ya Somalia, na inapinga kwa nguvu zote kuhamisha migogoro ya "Mashariki ya Kati" hadi eneo la Pembe ya Afrika.
-
Sheikh Ibrahim Zakzaky apinga pendekezo la Trump kuhusu Gaza
Aug 03, 2026 02:46Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu nchini Nigeria, Sheikh Ibrahim Zakzaky, amelitaja pendekezo la Rais wa Marekani Donald Trump kuhusu makubaliano ya usitishaji vita kati ya Israel na Hamas kuwa ni “uoga”, hasa kutokana na sharti linalodaiwa la kuitaka Hamas kusalimisha silaha zake.
-
TPLF ya Tigray yaituhumu serikali ya Ethiopia 'kuanzisha vita vya wazi'
Aug 02, 2026 13:02Mamlaka katika eneo la Tigray nchini Ethiopia zimeituhumu serikali ya shirikisho kuwa kuanzisha mashambulizi ya kijeshi siku ya Jumamosi, na kufufua hofu ya kurejea vitani.
-
Kitengo cha "Kundi 26" cha RSF chajisalimisha kwa jeshi la Sudan
Aug 02, 2026 02:45Shirika la Habari la Sudan SUNA limetangaza kuwa, kitengo kimoja cha Vikosi vya Usaidizi wa Haraka RSF kimejisalimisha kwa jeshi na kukabidhi wanajeshi wake na vifaa kamili vya kijeshi.
-
Ripoti ya polisi Kenya yafichua ukatili wa wanajeshi wa Uingereza Laikipia
Aug 01, 2026 11:45Ripoti ya siri ya polisi ya Kenya imefichua madai mazito ya ubakaji, ulawiti wa watoto na ukiukaji wa haki za kibinadamu unaodaiwa kufanywa na wanajeshi wa kikosi cha Uingereza wanaopata mafunzo Kenya (BATUK) katika Kaunti ya Laikipia.
-
Utafiti: Mlipuko wa Ebola Kongo ulianza miezi kadhaa kabla ya kugunduliwa
Aug 01, 2026 11:24Utafiti: Mlipuko wa Ebola Kongo ulianza miezi kadhaa kabla ya kugunduliwa
-
Rais wa Liberia awafukuta kazi maafisa kadhaa baada ya kukamatwa shehena kubwa za dawa za kulevya
Aug 01, 2026 06:31Rais Joseph Boakai wa Liberia amewafukuza kazi maafisa kadhaa wa serikali na huku akipendekeza kuchunguzwa baadhi ya maafisa kufuatia visa vingi vya dawa za kulevya katika miezi ya hivi karibuni ambavyo vimeibua malalamiko ya wananchi wakitaka hatua kali zichukuliwe.
-
Mvua kubwa yazingira maelfu ya watu katika kambi ya Al Karama 3 nchini Sudan, uhaba wa huduma waathiri familia
Aug 01, 2026 06:30Mvua kubwa za msimu zimezidisha hali mbaya kwa wakimbizi wa Sudan katika kambi ya Al Karama 3 huko Damazin, mji mkuu wa Jimbo la Blue Nile, ambayo imejaa watu zaidi ya 31,000 waliokimbia makazi yao kutokana na vita vya ndani.
-
Serikali ya Ghana yaunga mkono kuongezwa muhula wa urais kutoka miaka minne hadi mitano
Jul 31, 2026 10:17Serikali ya Ghana jana Alhamisi ilikubali pendekezo la kuongeza muhula wa urais kutoka miaka minne hadi mitano.
-
Waziri wa zamani Kenya: Rais Ruto anawalazimisha mawaziri kufanya anachotaka kwa woga
Jul 31, 2026 10:04Waziri wa zamani wa Fedha wa Kenya, Prof Njuguna Ndung’u, amemshutumu Rais wa nchi hiyo, William Ruto kwa kuingilia utendakazi wa taasisi huru, akisema mtindo huu umezorotesha uwezo wa kutekeleza majukumu ipasavyo.