-
Uingereza yashirikiana na Imarati kumiliki bandari ya Somaliland dhidi ya Sudan
Jan 10, 2026 23:02Serikali ya Uingereza imeripotiwa kumiliki bandari ya kimkakati inayodhibitiwa na Muungano wa Falme za Kiarabu (Imarati) katika eneo la Somaliland lililotangaza kujitenga la Somalia. Bandani hiyo ni sehemu ya mtandao wa miundombinu ya Imarati inayotumika kuvipelekea silaha Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF) vinavyofanya mauaji ya umati nchini Sudan.
-
Umoja wa Mataifa: Zaidi ya wakimbizi 50 wa Congo wamefariki Burundi
Jan 10, 2026 23:01Umoja wa Mataifa umetangaza kuwa, zaidi ya wakimbizi 50 wanaokimbia mapigano mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wamefariki duniani katika nchi jirani ya Burundi.
-
Wamorocco wachoma bendera ya Israel, wasisitiza kufutwa uhusiano wa kawaida na Tel Aviv
Jan 10, 2026 08:40Wananchi Morocco wameandamana na kukusanyika mbele ya bunge la nchi yao ambapo sambamba na kuchoma moto bendera ya utawala haramu wa Israel wametoa mwito kwa serikali ya nchi yao kufuta makubaliano ya kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala huo ghasibu.
-
Umoja wa Mataifa: Watu milioni 30 nchini Sudan wanahitajia msaada wa haraka
Jan 10, 2026 08:39Umoja wa Mataifa umetangaza kuwa, watu milioni 30 nchini Sudan wanahitajia msaada wa haraka wa kibinadamu.
-
Mkuu wa Baraza la Utawala Sudan: RSF itaangamizwa hivi karibuni
Jan 10, 2026 02:07Kiongozi wa Baraza la Utawala wa Mpito nchini Sudan amesema kuwa kundi la wapiganaji la Rapid Support Forces (RSF) litaangamizwa hivi karibuni.
-
Rais wa Jamhuri ya Afrika ya Kati amwalika Rais Putin baada ya ushindi
Jan 09, 2026 23:03Rais wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, Faustin-Archange Touadera, ambaye hivi karibuni ametangazwa mshindi katika uchaguzi wa rais, amemwalika Rais Vladimir Putin wa Russia kutembelea nchi hiyo jambo linaloashiria azma yake ya kushirikiana na Russia.
-
Nchi za Kiislamu zapinga safari za waziri wa Israel katika eneo la Somalia la 'Somaliland'
Jan 09, 2026 07:32Nchi 22 za Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) zimetoa taarifa na kutenga zinapinga vikali kujitenga eneo la Somaliland la Somalia huku zikilaani vikali safari ya waziri wa mambo ya nje wa utawala wa Kizayuni wa Israel katika eneo hilo.
-
Somalia yakanusha madai ya Marekani ya kutwaa chakula cha WFP
Jan 08, 2026 22:53Somalia jana Alhamisi ilikanusha madai ya Marekani kwamba maafisa wa eneo hilo wametwaa bidhaa za chakula kutoka katika ghala la shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP), huku Washington ikisimamisha misaada kwa Mogadishu kusubiri uchunguzi.
-
Afrika Kusini: Hatutazuia mpango wa Washington wa kuwapa hifadhi wazungu waliowachache
Jan 08, 2026 09:33Afrika Kusini imesema haitapinga mpango wenye utata wa serikali ya Washington wa kuwapeleka Marekani raia wazungu walio wachache wa Afrika Kusini.
-
Bobi Wine: Nitapitia upya mikataba ya mafuta ya Uganda iwapo nitachaguliwa Rais
Jan 08, 2026 09:18Bobi Wine mgombea mkuu wa upinzani katika uchaguzi wa kiti cha urais nchini Uganda uliopangwa kufanyika wiki ijayo, amesema kuwa atapitia upya makubaliano yaliyofikiwa kati ya nchi hiyo na makampuni ya mafuta duniani iwapo ataibuka na ushindi. Amesema ataifanyia marekebisho mikataba yoyote ambayo haina manufaa na maslahi kwa watu wa Uganda.