-
Tunisia: Ghannouchi na wenzake wahukumiwa kifungo cha maisha jela
Jun 03, 2026 13:16Mahakama ya Tunisia imemhukumu kifungo cha maisha jela kiongozi wa Harakati ya Ennahdha na Spika wa zamani wa Bunge, Rached Ghannouchi (miaka 84), pamoja na kuwahukumu wenzake katika kesi inayojulikana kwa jina la "Ennahdha Movement's Secret Apparatus".
-
Bunge la Zimbabwe lajadili rasimu ya muswada wa kuongeza muda wa urais
Jun 03, 2026 12:35Bunge la Zimbabwe linazingatia muswada tata wa marekebisho ya Katiba ambao utaongeza muhula wa Rais Emmerson Mnangagwa kwa miaka miwili hadi 2030.
-
Wanaharakati wa haki za binadamu waandamana Nairobi kupinga kituo cha Ebola cha Marekani nchini Kenya
Jun 02, 2026 15:14Wanaharakati wa kutetea haki za binadamu wamefanya maandamano leo mjini Nairobi wakipinga makubaliano yaliyofikiwa kati ya serikali ya nchi hiyo na Marekani ya kuanzisha nchini Kenya kituo cha kuhifadhi Wamarekani wanaoshukiwa kuambukizwa virusi vya Ebola.
-
Visa vya Ebola vimefika 300 nchini DR Congo huku maeneo zaidi ya afya yakiathirika
Jun 02, 2026 09:06Idadi ya visa vilivyothibitishwa vya ugonjwa wa Ebola katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) imevuka 300 kufikia Jumatatu.
-
Raia watano wa Msumbiji wauawa katika ‘Mashambulizi ya Chuki’ nchini Afrika Kusini
Jun 02, 2026 09:01Serikali ya Msumbiji imetangaza kuwa takriban raia wake watano wameuawa katika “mashambulizi ya chuki dhidi ya wageni” nchini Afrika Kusini mwishoni mwa juma lililopita. Vifo hivyo vinaashiria kushadidia maandamano yanayoendelea nchi nzima dhidi ya wahamiaji wasio na vibali.
-
Walimu Nigeria waitisha mgomo katika jimbo la Oyo kufuatia vitendo vya utekaji nyara shuleni
Jun 02, 2026 02:53Muungano wa Walimu wa Nigeria umeitisha mgomo wa wazi kuanzia leo Jumatatu katika jimbo la Oyo kupinga kutekwa nyara makumi ya watoto na walimu wao katikati ya mwezi wa Mei mwaka huu.
-
Jeshi la Somalia lamuuwa kamanda mwandamizi wa kundi la kigaidi la Al Shabaab
Jun 02, 2026 02:51Jeshi la Taifa la Somalia (SNA) limewaua wanachama wawili wa kundi la kigaidi la Al Shabaab, akiwemo kamanda mwandamizi, katika operesheni ya kijeshi iliyopangwa katika eneo la Hanti Wadaag, mkoani Lower Shabelle.
-
Rais Ruto aagiza ujumuishaji wa Shule za Kiislamu katika mfumo rasmi wa elimu wa Kenya
Jun 01, 2026 13:06Rais wa Kenya, William Ruto, amemwagiza waziri wa elimu kushirikisha wadau wote husika na kuanzisha mashauriano kuhusu ujumuishaji rasmi wa shule za Kiislamu nchini, zinazojulikana kama Duksi au Madrasa, katika mfumo wa elimu wa Kenya.
-
Wanawake wako katika hatari kubwa ya kuathiriwa na mlipuko wa Ebola Kongo
Jun 01, 2026 11:44Wakati Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ikiendelea na mapambano dhidi ya maambukizi ya ugonjwa wa Ebola, wanawake nchini humo wametajwa kuwa kundi lililo kwenye hatari ya kuambukizwa ugonjwa huo unaosababishwa na virusi.
-
Uchaguzi mkuu Ethiopia; Abiy Ahmed anatarajiwa kushinda tena kiti cha Waziri Mkuu
Jun 01, 2026 02:42Uchaguzi mkuu wa Ethiopia unatarajiwa kufanyika Jumatatu hii huku migogoro ikiendelea katika baadhi ya maeneo ya nchi, ikimaanisha kuwa watu wengi hawataweza kupiga kura.