-
Miili 460 ya watu yapatikana hospitalini El Fasher, mawaziri wa Sudan na Misri wakutana
Oct 30, 2025 06:46Zaidi ya wagonjwa 460 na watu walioandamana nao wameripotiwa kupatikana wameuawa katika hospitali ya uzazi huku kukiwa na ripoti za kuendelea ukatili dhidi ya raia huko El Fasher, Sudan. Hayo yameripotiwa huku mawaziri wa Mambo ya Nje wa Sudan na Misri wakikutana kujadiliana hali ya eneo hilo la magharibi mwa Sudan.
-
Angola yatangaza kuwekeza kwenye satelaiti mpya
Oct 30, 2025 06:46Serikali ya Angola imetangaza kuwa itaongeza uwekezaji katika sekta ya mawasiliano ya simu, ambao utajumuisha mpango wa kurusha satelaiti mpya ya uchunguzi na kupanua mtandao wa taifa wa mawasiliano kama sehemu ya mkakati mpana wa kufaidika vizuri na teknolojia za kisasa zinazojumuisha watu wote nchini humo.
-
Iran yaanza majaribio ya safari za ndege za mizigo zilizotengenezwa nyumbani
Oct 30, 2025 02:26Ndege ya Simorgh iliyotengenezwa Iran imeanza rasmi safari zake za majaribio huku ikijiandaa kujiunga na sekta ya usafirishaji mizigo hapa nchini.
-
Uchaguzi Mkuu Tanzania waendelea kwa amani licha ya machafuko ya hapa na pale
Oct 29, 2025 15:31Shughuli za upigaji kura katika Uchaguzi Mkuu wa Tanaznia zimeendelea vizuri na kwa amani kwa kikasi kikubwa licha ya ghasia na machafuko madogo yanayoripotiwa huku na kule.
-
Ripoti: UAE inawapa waasi wa RSF silaha kutoka Uingereza
Oct 29, 2025 09:51Katika kile kinachoibua maswali mazito kuhusu usafirishaji wa silaha na ushawishi wa mataifa ya nje katika vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Sudan, ripoti mpya imefichua kuwa Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) imewasambazia waasi wa RSF silaha na vifaa vya kijeshi vilivyotengenezwa Uingereza.
-
Ripoti ya Umoja wa Afrika: Tanzania yaongoza uchumi wa kanda, Kenya na Rwanda zikiachwa nyuma
Oct 29, 2025 09:09Uchumi wa Kenya umeendelea kusuasua ikilinganishwa na ule wa Tanzania katika eneo la Afrika Mashariki, hasa kutokana na utegemezi mkubwa wa mauzo ya bidhaa ghafi nje ya nchi jambo linalokwamisha ukuaji wa uchumi na kuongeza kiwango cha umaskini.
-
IOM: Zaidi ya raia 7,400 wamekimbia makazi yao huko El-Fasher, Sudan
Oct 29, 2025 07:31Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM) limeeleza kuwa watu wasiopungua 7,455 wamekimbia imji wa El fasher magharibi mwa Sudan katika muda wa siku moja kufuatia mashambulizi ya wanamgambo wa Kikosi cha Msaada wa Haraka (RSF).
-
Mjumbe wa UN: Mchakato wa amani nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati 'umepiga hatua'
Oct 29, 2025 07:29Mwakilishi wa ngazi ya juu wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR) ameeleza kuwa mchakato wa amani umepiga hatuua kufuatia makubaliano ya kusitisha mapigano yaliyosainiwa mwezi Aprili hata hivyo ametahadharisha kuwa kupunguzwa kwa bajeti ijayo kunaweza kudhoofisha mchakato huo.
-
Serikali ya Madagascar yatangaza baraza la mawaziri
Oct 29, 2025 07:28Serikali ya Madagascar inayoongozwa na jeshi leo imetangaza baraza la mawaziri linalojumuisha idadi kubwa ya mawaziri wa kiraia.
-
Watanzania leo wanamchagua Rais, Wabunge na madiwani
Oct 29, 2025 03:02Watanzania waliotimiza masharti ya kupiga kura leo wanaelekea katika vituo vya kupigia kura kwa ajili ya kumchagua Rais, Wabunge na madiwani katika uchaguzi uliosusiwa na chama kikuu cha upinzani cha CHADEMA.