-
Mjumbe wa UN: Mchakato wa amani nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati 'umepiga hatua'
Oct 29, 2025 07:29Mwakilishi wa ngazi ya juu wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR) ameeleza kuwa mchakato wa amani umepiga hatuua kufuatia makubaliano ya kusitisha mapigano yaliyosainiwa mwezi Aprili hata hivyo ametahadharisha kuwa kupunguzwa kwa bajeti ijayo kunaweza kudhoofisha mchakato huo.
-
Serikali ya Madagascar yatangaza baraza la mawaziri
Oct 29, 2025 07:28Serikali ya Madagascar inayoongozwa na jeshi leo imetangaza baraza la mawaziri linalojumuisha idadi kubwa ya mawaziri wa kiraia.
-
Watanzania leo wanamchagua Rais, Wabunge na madiwani
Oct 29, 2025 03:02Watanzania waliotimiza masharti ya kupiga kura leo wanaelekea katika vituo vya kupigia kura kwa ajili ya kumchagua Rais, Wabunge na madiwani katika uchaguzi uliosusiwa na chama kikuu cha upinzani cha CHADEMA.
-
Senegal yachunguza mauaji ya kikoloni ya Ufaransa baada ya uchimbaji mpya, Thiaroye
Oct 28, 2025 17:55Wanaakiolojia nchini Senegal wamegundua ushahidi mpya wa mauaji ya kikoloni ya Ufaransa yaliyotokea mwaka 1944, kama sehemu ya juhudi zinazoongozwa na serikali za kufichua ukweli kuhusu mauaji yaliyofanywa na vikosi vya jeshi la Ufaransa baada ya Vita vya Pili vya Dunia dhidi ya ya wanajeshi wa Afrika Magharibi.
-
Mgogoro wa El Fasher: Maelfu wakadiriwa kuuawa, Umoja wa Afrika walaani "ukatili"
Oct 28, 2025 12:22Waziri wa Afya katika jimbo la Darfur, Babiker Hamdeen amesema kwamba maelfu ya raia wameuawa katika mji wa El Fasher katika siku mbili zilizopita, huku Umoja wa Afrika ukilaani "ukatili" na "madai ya kufanyika uhalifu wa kivita" huko El Fasher, magharibi mwa Sudan.
-
Maandamano ya Tunisia na Morocco; dhihirisho la kuunga mkono Wapalestina barani Afrika
Oct 28, 2025 11:45Wimbi jipya la uungaji mkono kwa Wapalestina barani Afrika limekwenda sambamba na kulaani vitendo vya kijinai vya utawala haramu wa Israel.
-
Ajali ya ndege yaua 12 Kenya wakiwemo watalii wa kigeni
Oct 28, 2025 11:32Watu 12, wakiwemo watalii, wanahofiwa kufariki dunia katika ajali ya ndege iliyotokea katika eneo la Vyungwani, Matuga, Kaunti ya Kwale, mapema leo Jumanne.
-
Watu wenye hasira waendelea kuandamana Cameroon kupinga ushindi wa Paul Biya
Oct 28, 2025 09:12Maeneo mbalimbali ya Cameroon yameendelea kushuhhudia maandamano ya watu wenye hasira wanaopinga matokeo ya uchaguzi yaliyompa ushindi rais kizee zaidi duniani yaani Paul Biya mwenye umri wa miaka 92.
-
OHCHR: Waasi wa RSF wamefanya ukatili wa kutisha nchini Sudan
Oct 28, 2025 07:56Ofisi ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa OHCHR imesema imepokea taarifa za kutisha kuwa waasi wa RSF wanafanya ukatili wa kutisha nchini Sudan.
-
Uchaguzi wa mapema unafanyika Zanzibar leo
Oct 28, 2025 07:53Leo, visiwa vya Zanzibar vimeingia katika hatua muhimu ya mchakato wa uchaguzi kwa kuanza rasmi zoezi la kupiga kura ya mapema, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya uchaguzi mkuu wa Tanzania unaotarajiwa kufanyika kesho, Oktoba 29, katika Tanzania Bara na visiwani.