Muungaji mkono Palestina aapishwa kuwa Rais mpya wa Ireland
https://parstoday.ir/sw/news/world-i133116-muungaji_mkono_palestina_aapishwa_kuwa_rais_mpya_wa_ireland
Bi. Catherine Connolly, mgombea wa mrengo wa kushoto katika uchaguzi wa urais nchini Ireland ambaye anajulikana kwa misimamo yake ya kuunga mkono Palestina, ameapishwa kuwa rais mpya wa Ireland baada ya kuibuka mshindi katika uchaguzi wa mwezi uliopita.
(last modified 2025-11-13T07:16:27+00:00 )
Nov 13, 2025 07:16 UTC
  • Muungaji mkono Palestina aapishwa kuwa Rais mpya wa Ireland
    Muungaji mkono Palestina aapishwa kuwa Rais mpya wa Ireland

Bi. Catherine Connolly, mgombea wa mrengo wa kushoto katika uchaguzi wa urais nchini Ireland ambaye anajulikana kwa misimamo yake ya kuunga mkono Palestina, ameapishwa kuwa rais mpya wa Ireland baada ya kuibuka mshindi katika uchaguzi wa mwezi uliopita.

Rais wa Kumi wa Ireland ameanza rasmi muhula wake katika hali ambayo sera zake zimeibua wasiwasi barani Ulaya na utawala wa Kizayuni hasa kutokana na misimamo yake imara ya kuunga mkono Palestina.

Mwanamama huyo ni mkosoaji mkubwa wa utawala wa Kizayuni, Umoja wa Ulaya na Jumuiya ya Kujihami ya NATO na muungaji mkono wa Palestina.

Akizungumza katika sherehe za kuapishwa rasmi kuwa rais: Catherine Connolly alisema: "Lazima tufanye juhuudi za kusimamisha vita, vita vinavyoendelea sambamba na mauaji ya halaiki, uzoefu wa kukoloniwa na kusimama kidete kuukabiliana nao, pamoja na njaa ambayo iliundwa kwa ajili yetu, inatupa uwezo wa kuelewa kwa usahihi na kuelewa watu waliohama, njaa na vita."

Connolly, (68), alifanikiwa kushinda kwa asilimia 63 ya kura akipata uungaji mkono mkubwa kutoka kwa vijana wa Ireland. Katika masuala ya sera za nje, amekuwa mwanasiasa mwenye msimamo thabiti wa kuunga mkono Palestina, huku akionyesha ukosoaji mkali dhidi ya Umoja wa Ulaya na Marekani.

Katika chapisho la hivi karibuni aliloweka kwenye Instagram, Rais Connolly aliandika: “Israel imefanya mauaji ya kimbari huko Gaza. Kuona au kufanya mauaji ya kimbari kuwa jambo la kawaida ni janga kubwa kwa watu wa Palestina na ni janga kwa ubinadamu wote.”