-
Uchaguzi wa rais wa Iran waingia duru ya pili, Wairani kupata rais mpya baada ya Ijumaa ijayo
Jun 29, 2024 04:37Matokeo rasmi na ya mwisho ya duru ya 14 ya uchaguzi wa rais wa kabla ya wakati wa Iran yanaonesha kuwa zoezi hilo limeingia katika duru ya pili.
-
Serikali ya Biden yakiri kudumisha siasa za vikwazo dhidi ya Iran
Jun 28, 2024 22:55Matthew Miller, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani, alitangaza katika mkutano na waandishi wa habari siku ya Jumatano sambamba na siasa za undumakuwili za Washington kuhusu wananchi wa Iran, kwamba nchi hiyo ya imeweka vikwazo zaidi ya 600 dhidi ya serikali na mashirika ya Iran.
-
Macron aonya kuhusu uwezekano wa kutokea vita vya ndani nchini Ufaransa
Jun 28, 2024 08:57Katika mkesha wa uchaguzi wa mapema wa Bunge, Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron ameonya kuhusu uwezekano wa kupata ushindi makundi ya mrengo wa kushoto na kulia yenye misimamo ya kufurutu mipaka na kutokea vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini humo.
-
Siasa za kindumakuwili za Biden kuhusu vita vya Gaza
Jun 27, 2024 23:48Harrison Mann, afisa wa ujasusi katika jeshi la Marekani, ambaye alijiuzulu karibuni katika kupinga uungaji mkono wa Washington kwa utawala wa Kizayuni katika vita vyake vya mauaji ya umati dhidi ya watu wa Palestina huko Gaza, aliiambia Al Jazeera ya Qatar siku ya Jumanne usiku kwamba: "Kama usingekuwa uungaji mkono wa Marekani kwa Israel, vita vya Gaza visingeliendelea kwa nguvu hizi."
-
Kuongezeka kasi katika ushirikiano wa kimkakati kati ya Iran na Russia
Jun 27, 2024 08:55Uhusiano na ushirikiano wa kistratijia kati ya Iran na Russia umeongezeka na kushika kasi zaidi katika siku za hivi karibuni, na sasa unaingia katika hatua mpya.
-
Kutoweka watoto katika Ukanda wa Gaza
Jun 26, 2024 22:59Kwa mujibu wa ripoti mpya zilizochapishwa na shirika la kimataifa linaloitwa "Save the Children", watoto wapatao elfu 21 wa Kipalestina wametoweka huko Ukanda wa Gaza, ambapo watoto elfu 17 wametenganishwa na familia zao kutokana na vurugu zilizosababishwa na vita, hasa operesheni za hivi karibuni za utawala wa Kizayuni katika ukanda huo.
-
Ushiriki wa kiwango cha juu zaidi; mkakati wa kudumu wa Kiongozi wa Mapinduzi kuhusu uchaguzi
Jun 26, 2024 05:48Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameashiria uchaguzi muhimu sana wa siku ya Ijumaa (28 Juni), na kusisitizia ushiriki wa kiwango cha juu kabisa wa wananchi na kuwataka wananchi wa taifa hili kujitokeza katika vituo vya kupigia kura Ijumaa ya keshokutwa ili kumchagua Rais mpya.
-
Tehran, mwenyeji wa Jumuiya ya Mazungumzo ya Ushirikiano wa Asia (ACD).
Jun 25, 2024 22:47Kikao cha 19 cha Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Jumuiya ya Mazungumzo ya Ushirikiano wa Asia (ACD) kilifanyika Jumatatu hapa mjini Tehran chini ya uenyekiti wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
-
Kuendelea mivutano kati ya Netanyahu na jeshi la Kizayuni
Jun 25, 2024 08:51Vita vya Gaza vimeingia katika mwezi wa tisa huku mizozo na mivutano kati ya Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, na maafisa wa kijeshi wa utawala wa Kizayuni ikiendelea kushika kasi.
-
Makubaliano ya kuanzisha mazungumzo kati ya Tehran na Manama, ishara ya mafanikio ya siasa za nje za Iran
Jun 24, 2024 07:33Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Bahrain zimetoa taarifa ya pamoja zikielezea kuwekwa mikakati muhimu ya kuanzisha mazungumzo baina ya nchi mbili kwa lengo la kuchunguza namna ya kurejesha uhusiano wa kisiasa. Taarifa hii ya pamoja imetolewa kufuatia mazungumzo yaliyofanyika karibuni kati ya Ali Bagheri Kani, Kaimu Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Waziri mwenzake wa Mashauri ya Kigeni wa Bahrain.