-
Russia yakosoa mwenendo wa kinafiki wa Marekani kuhusu masuala ya anga
Nov 18, 2021 23:23Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia amezitaja tuhuma za Marekani dhidi ya Moscow kwamba inatumia silaha dhidi ya satalaiti na kusababisha vitisho angani kuwa ni za kinafiki na zisizo na ukweli wowote. Sergey Lavrov amesema kuwa: "Tunaona kwkamba, badala ya kutoa madai yasiyo na msingi wowote, ni vyema Marekani iketi kwenye meza ya mazungumzo na ieleze mitazamo yake kuhusu makubaliano yaliyopendekezwa na Russia na China kwa ajili ya kuzuia mashindano ya silaha angani
-
Mchango wa vijana wenye vipaji na viwapa vya juu katika mtazamo wa Kiongozi Muadhamu
Nov 18, 2021 09:58Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu jana Jumatano alihutubia hadhara ya vijana wenye viwapa na vipaji vikubwa vya kieleimu akisisitiza udharura wa jamii ya wasomi kujikita katika suala la kupata njia za kisayansi za kutatua matatizo mbalimbali.
-
Jinai ya kivita ya mamluki wa Saudi Arabia dhidi ya mateka wa kivita nchini Yemen
Nov 17, 2021 23:25Muungano vamizi unaoongozwa na Saudi Arabia huko Yemen siku za karibuni uliwanyonga mateka 10 wa kivita wa jeshi la Yemen. Wizara ya Mambo ya Nje ya Serikali ya Wokovu wa Kitaifa ya Yemen imesema kuwa hatua hiyo ni jinai ya kivita.
-
Mazungumzo ya Marais wa Iran na Russia, sisitizo la kustawisha zaidi uhusiano na ushirikiano wa nchi mbili
Nov 17, 2021 06:11Rais Vladimir Putin wa Russia amefanya mazungumzo ya simu na Rais Sayyid Ebrahim Raisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na kuashiria mwelekeo chanya wa kupandisha juu kiwango cha ushirikiano wa pande mbili, kieneo na kimataifa na kueleza kuwa, mchakato wa kustawisha ushirikiano utapiga hatua kwa kasi kubwa zaidi.
-
Sababu za mamluki wa Saudia na Imarati kuondoka magharibi mwa Yemen
Nov 16, 2021 22:59Katika siku za hivi karibuni kumeshuhudiwa vikosi vya muungano vamizi wa Saudi Arabi-Imarati vikiondoka katika ngome zao katika mji wa bandari wa al-Hudaydah.
-
Kuimarishwa uhusiano wa Iran na Uturuki; kuelekea kwenye kiwango cha ushirikiano wa pande zote
Nov 16, 2021 04:21Jumatatu ya jana tarehe 15 Novemba, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Uturuki alikutana na kufanya mazungumzo hapa mjini Tehran na Rais Ibrahim Raeisi na Hussein Amir-Abdollahian, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
-
Malengo ya kisiasa ya mazoezi ya kijeshi ya Israel na nchi kadhaa za Kiarabu
Nov 15, 2021 23:00Mazoezi ya kijeshi ya utawala wa Kizayuni wa Israel yameongezeka sana katika siku za karibuni. Wachambuzi wa mambo wanaamini kuwa, mazoezi hayo ya kijeshi ni kielelezo cha wasiwasi wa usalama wa Israel na woga wa utawala huo kutokana na kambi ya mapambano na kwamba yanafanyika kwa malengo ya kisiasa.
-
Kuendelea mgogoro wa kisiasa nchini Sudan
Nov 15, 2021 10:35Maandamano ya kupinga mapinduzi yaliyofanywa na Jeshi la Sudan dhidi ya serikali ya mpito ya nchi hiyo yangali yanaendelea huku wananchi wakitaka kurejeshwa madarakani serikali ya kiraia. Sambamba na hayo ripoti iliyotolewa Jumatatu na Tume ya Madaktari wa Sudan inasema idadi ya watu waliouawa kwa kupigwa risasi na wanajeshi katika maandamano ya Jumamosi iliyopita imefikia watu 8.
-
Madai ya Taliban ya kuwepo serikali jumuishi nchini Afghanistan
Nov 14, 2021 23:16Kaimu waziri wa mambo ya nje wa serikali ya muda ya Taliban amekataa wito wa jamii ya kimataifa unaosisitizia ulazima wa kuundwa serikali jumuishi nchini Afghanistan na kudai kwamba, serikali ya Taliban ni jumuishi na ndani yake wamo wawakilishi wa jamii zote za nchi hiyo.
-
Kufichuliwa jinai za kivita za jeshi la Marekani nchini Syria
Nov 14, 2021 07:42Gazeti la New York Times limetoa ripoti inayoonyesha kuwa, jeshi la Marekani limetenda uhalifu wa kivita kwa kuua makumi ya wanawake na watoto katika mashambulio ya anga liliyofanya nchini Syria kwa kisingizio cha kile kinachoitwa mapambano dhidi ya kundi la DAESH (ISIS).