-
Mufti wa Tanzania awahimiza Waislamu kujifunza sayansi + Sauti
Nov 11, 2018 14:03Mufti wa Tanzania, Sheikh Abubakari Zuberi bin Ali amewataka Waislamu wa Tanzania kujiendeleza na kujitanua katika nyanja mbalimbali za kielimu hasa katika sekta ya sayansi na teknologia ili kuiendeleza dini ya Kiislamu kwa njia bora zaidi. Ammari Dachi na taarifa zaidi kutoka Dar es Salaam...
-
SAUTI, Serikali ya Uganda yashauriwa kuzidisha juhudi za kivitendo katika kukuza lugha ya Kiswahili nchini
Nov 09, 2018 13:40Serikali ya Uganda imeshauriwa kuongeza juhudi kwa ajili ya ufundishaji lugha ya Kiswahili kwa madaraja yote ya elimu nchini humo.
-
SAUTI, Uhaba wa nishati ya mafuta nchini Congo Brazzaville wayafanya maisha ya wananchi kuwa magumu mno
Nov 09, 2018 12:42Jiji la Brazzaville nchini Kongo, limekumbwa na uhaba mkubwa wa nishati ya mafuta ya petrol na hivyo kuyafanya maisha ya wakazi wa mji huo na miji mingine ya jirani kuwa magumu.
-
Serikali ya Tanzania yaahidi kutafuta soko la uhakika la korosho + Sauti
Nov 08, 2018 13:10Serikali ya Tanzania imewataka wananchi hususan wakulima wa korosho nchini humo kuendelea kuwa watulivu wakati ikiendelea kuongea na wanunuzi wakubwa wa korosho kutoka maeneo mbalimbali duniani ili kupata masoko ya uhakika wa zao hilo. Amari Dachi na maelezo zaidi kutoka Dar es Salaam...
-
Rais Uhuru Kenyatta alipongeza jeshi la Kenya kwa kazi nzuri linayoifanya + Sauti
Nov 08, 2018 13:07Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya amepongeza juhudi za jeshi la nchi yake KDF kujumlisha tekinolojia ya kisasa katika mfumo wake wa utoaji mafunzo kwa makuruta, akiitaja hatua hio kama chanya kwenye kuafiki kasi ya mabadiliko ya changamoto za kiusalama nchini mwake na Pembe ya Afrika. Seifullah Murtadha na maelezo zaidi...
-
Video: Waislamu wa Kisuni Iran waungana na ndugu zao wa Kishia kufanya ziara katika Haram ya Imam Ridha
Nov 06, 2018 08:11Wanavuoni, vijana na Waislamu wa matabaka mbalimbali wa Iran wameungana na ndugu zao wa Kishia kufanya ziara katika Haram ya Imam Ridha AS, mmoja wa wajukuu wa Bwana Mtume Muhammad SAW ambaye pia ni Imam wa Nane wa Waislamu wa Kishia.
-
Bunge la Afrika lamaliza vikao vyake nchini Rwanda + Sauti
Nov 06, 2018 03:28Bunge la Afrika limekamilisha vikao vyake vya wiki mbili mjini Kigali Rwanda kwa kuanzisha tunzo maalumu ya uongozi bora barani Afrika kwa hisani ya hayati Kofi Annan, Katibu Mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa. Mwandishi wetu Sylvanus Karemera na ripoti zaidi...
-
Vita dhidi ya ufisadi Kenya, asasi za kijamii zaiandalia chata Serikali + Sauti
Nov 06, 2018 03:25Asasi za kijamii nchini Kenya zimeweka mikakati ya kubadilisha taswira kwenye vita dhidi ya ufisadi kwa kuandaa chata ambayo inaielekeza serikali katika kupambana na ugaidi bila ya kutumia nguvu kupita kiasi. Seifullah Murtadha na taarifa zaidi...
-
Wakazi wa Kivu Kaskazini waomboleza mauaji ya wenzao yaliyofanywa na Jenerali Nkunda Batware + Sauti
Nov 06, 2018 03:12Wakazi wa eneo moja la mkoa wa Kivu Kaskazini huko Kongo DR wamekumbuka miaka kumi tangu walipouliwa raia wenzao na wanamgambo wa Jenerali Laurent Nkunda Batware na wametaka kuundwe tume ya kuchunguza mauaji hayo. Mossi Mwassi na taarifa zaidi...
-
DRC yalalamikia uingiliaji wa Marekani katika uchaguzi wa nchi hiyo + Sauti
Nov 05, 2018 03:49Viongozi wa Jamhuri ya Kidemokrsia ya Kongo wamelalamikia ripoti mpya ya Chuo kikuu cha New York cha nchini Marekani kilichodai kuwa Uchaguzi Mkuu wa mwezi ujao wa Disemba huko DRC utakuwa wa hatari zaidi kuliko hata inavyotarajiwa. Mwandishi wetu Mossi Mwassi na maelezo zaidi kutoka mjini Brazzaville.