Abdollahian: Uwepo wa vikosi vya kigeni katika ardhi ya Syria si ufumbuzi
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i100532-abdollahian_uwepo_wa_vikosi_vya_kigeni_katika_ardhi_ya_syria_si_ufumbuzi
Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, uwepo wa vikosi vya kigeni katika ardhi ya Syria hakusaidii katu amani na uthabiti wa nchi hiyo wala wa eneo la Asia Magharibi.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jul 31, 2023 10:13 UTC
  • Abdollahian: Uwepo wa vikosi vya kigeni katika ardhi ya Syria si ufumbuzi

Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, uwepo wa vikosi vya kigeni katika ardhi ya Syria hakusaidii katu amani na uthabiti wa nchi hiyo wala wa eneo la Asia Magharibi.

Hussein Amir-Abdollahian, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema hayo leo hapa mjini Tehran katika mazungumzo na waandishi wa habari akiwa na Faisal Miqdad, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Syria na kueleza kwamba, Tehran itaendeleza kwa nguvu zake zote juhudi na uungaji mkono wake kwa ajili ya kuhakikisha amani na usalama wa kudumu unapatikana katika eneo.

Abdollahian amelaani hujuma na mashambulio ya mara kwa mara ya utawala haramu wa Israel dhidi ya ardhi ya Syria na kueleza kwamba, Israel ndio chimbuko kuu la ukosefu wa usalama na amani kwani utawaa huo untambua kuwa ili ubakkie basi unapaswa kuendesha vita.

Mawaziri wa Mashauri ya Kigeni wa Iran Hussein Amir-Abdollahian (kulia) na Faisal Miqdad wa Syria

 

Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Iran amesema kuwa, mataifa ya eneo hayatapuuza harakati za Israel na kwamba, watawala bandia wa utawala ghasibu wa Israel wamediriki na kutambua kwamba, hakuna hatua yoyote ya Wazayuni ambayo itabakia hivi hivi bila ya majibu.

Kwa upande wake, Faisal Miqdad Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Syria sambamba na kubainisha kwamba, hakuna uadui wowote baina ya Syria na Uturuki amesema, vikosi vya kigeni vinapaswa kuondoka katika ardhi ya Syria.

Aidha amesifu na kuthamini himaya na uungaji mkono wa Iran kwa Syria na kueleza kwamba, Tehran imefanya juhudi kubwa za kuiunga mkono Syria kiuchumi, mafuta, gesi na misaada ya kibinadamu.