Feb 02, 2024 02:42 UTC
  • Spika ya Majlisi ya Iran: Utamaduni wa kufa shahidi unawatia hofu maadui

Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran (Bunge) ameeleza kuwa utamaduni wa kufa shahidi unawatia hofu maadui.

Muhammad Bagher Qalibaf amechambua shakhsia ya kiakhlaqi na ya kijasiri ya shahidi Brigedia Jenerali Sayyid Razi Mousavi na kueleza kuwa utamaduni wa kufa shahidi ni  utamaduni asili wa Kiislamu ambao siku zote unawatia hofu maadui.  

Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran alibainisha haya jana mjini Tehran katika marasimu ya  arobaini  ya shahidi Brigedia Jenerali Sayyid Razi Mousavi. 

Shahidi Mousavi Razi

Qalibaf ameongeza kuwa: Maadui wanapasa kujua kwamba shahidi Sayyid Razi Mousavi bila shaka alikuwa akihudumia mhimili wa muqawama, na alikuwa akitambulika kama mmoja wa nguzo za mhimili mhimili huo; na akasema: maadui kamwe  wasifikirie kuwa nguzo hii imeanguka, bali itazidi kuimarika siku baada ya siku. 

Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu pia ameashiria nafasi ya Luteni Jenerali shahidi Qassim Suleimani aliyekuwa Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) miongoni mwa wananchi wa Iran na pia katika mataifa ya Kiislamu na wapigania ukombozi duniani na kusema: Tafakari zote hizi zinatokana na utamaduni wa kufa shahidi na baraka za Mapinduzi ya Kiislamu. 

Brigedia Jenerali Sayyid Razi Mousavi aliyekuwa kati ya washauri wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu huku akifanya kazi katika uwanja wa kuunga mkono mhimili wa muqawama huko Syria aliuawa shahidi katika shambulio la kigaidi la utawala wa Kizayuni Desemba 25 mwaka jana kwenye eneo la Zainabiyah huko Damascus mji mkuu wa Syria. 

Tags