Apr 17, 2024 03:28 UTC
  • Brigedia Jenerali Kioumars Haydari
    Brigedia Jenerali Kioumars Haydari

Kamanda wa Kikosi cha Nchi Kavu cha Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Brigedia Jenerali Kioumars Haydari amesema operesheni ya kulipiza kisasi ya Iran dhidi ya utawala haramu wa Israel imeondoa zaidi dhana potofu kwamba utawala huo khabithi na muuaji watoto hauwezi kushindwa.

Jenerali Haydari alisema siku ya Jumanne kwamba, mafanikio ya kurushwa kwa mamia ya makombora na ndege zisizo na rubani kuelekea Israel ili kulipiza kisasi shambulio la kigaidi la utawala wa Israel la tarehe 1 Aprili katika ubalozi mdogo wa Jamhuri ya Kiislamu nchini Syria ni jibu kali kwa utawala katili wa Israel.

Haydari alisisitiza zaidi kwamba shambulio la kulipiza kisasi la Iran lililenga kituo cha kistratijia zaidi cha jeshi la Israel katika Miinuko ya Jabal al-Sheikh kwenye mpaka kati ya ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu na Syria.

Ameongeza kuwa: "Shambulio kwenye kituo hicho na kituo cha jeshi la anga cha, ambacho kinashehehni zana za kivita za kimkakati vya utawala wa Kizayuni, ni kipigo kikubwa  kwa uwezo wa kijeshi wa utawala huo."

Aidha Haydari amesema katika mkutano na waandishi wa habari mjini Tehran kwa mnasaba wa Siku ya Jeshi la Kitaifa, ambayo huadhimishwa kila mwaka Aprili 18, kwamba utawala wa Israel utapata jibu kali zaidi iwapo utaamua kutekeleza uchokozi mpya dhidi ya. Iran.