Apr 30, 2024 11:14 UTC
  • Ujumbe wa Algeria na azma yake ya kustawisha ushirikiano wa kiteknolojia na Iran

Mkuu wa Chama cha Wafanyabiashara wa Algeria amepongeza maendeleo ya kiteknolojia ya Iran na kusisitiza azma ya nchi hiyo ya kuendeleza ushirikiano wa kiteknolojia na Iran.

Kamal Himani, Mkuu wa Chama cha Wafanyabiashara wa Algeria, ambaye yuko hapa Tehran akiongoza ujumbe wa wafanyabiashara wa nchi hiyo kwa lengo la kushiriki katika Maonesho ya Iran amepongeza uwezo wa makampuni ya  Iran yanayotegemea sayansi na teknolojia na akasema amefurahishwa kutembelea mafanikio ya Iran. Hamani amesisitiza kuwa ziara yake katika Nyumba ya Ubunifu na Teknolojia ya Iran imeimarisha azma ya Algeria ya kuendeleza ushirikiano na Iran. 

Mkuu wa Chama cha Wafanyabiashara wa Algeria ameongeza kuwa mbali na teknolojia ya hali ya juu; azma ya Algeria ya kustawisha ushirikiano na Iran imeongezeka zaidi kutokana na miamala mizuri na ikhlasi ya Wairani. 

Kamal Himani ameeleza kuwa wawakilishi wa Algeria wameshuhudia kuwau tayari Iran kuhamishia teknolojia yake katika pembe zote za dunia na wamestaajabishwa sana na kiwango cha utayarifu wa Iran. 

Jamhuri ya Kiislamu ya Iran haizitazami tu nchi za Ulaya katika fremu ya ushirikiano wake mkubwa na nchi mbalimbali duniani; bali Jamhuri ya Kiislaamu ya Iran inatilia mkazo kushirikiana na nchi za bara la Afrika na Asia pia. 

Soko kubwa la Afrika ni jukwaa kwa ajili ya kuuza bidhaa za Iran 

Soko kubwa la Afrika ni jukwaa linalofaa kwa ajili ya kuuza bidhaa za Iran; na katika hali hiyo, bara la Afrika lina nafasi maalum katika siasa za nje za Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Tags