Ghuba ya Uajemi; nembo ya ukweli wa kihistoria usiokanushika
(last modified 2024-07-09T02:23:41+00:00 )
Jul 09, 2024 02:23 UTC
  • Ghuba ya Uajemi; nembo ya ukweli wa kihistoria usiokanushika

Balozi na mwakilishi wa kudumu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika Umoja wa Mataifa ameliandikia barua Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa  akijibu msimamo wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu (Arab League) kuhusiana kuheshimiwa ardhi yote ya Iran na kutopotoshwa jina la Ghuba ya Uajemi.

Katika barua yake hiyo, Amir Saeid Iravani Balozi na Mwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika Umoja wa Mataifa amelaani vikali na kukadhibisha tuhuma za uwongo na zisizo na msingi dhidi ya mamlaka ya kujitawala na umoja wa ardhi nzima ya Iran zilizobainishwa katika kifungu cha 11 cha taarifa ya Jumuiya ya Nchi za Kiarabu.

Balozi Iravani amezitaja tuhuma hizo dhidi ya Iran kuwa ni uingiliaji wa wazi na usio wa kiadilifu katika masuala ya ndani ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Barua hiyo ya Balozi wa Iran katika Umoja wa Mataifa imeeleza kuwa, taarifa iliyotolewa na nchi za Kiarabu dhidi ya Iran si tu kuwa ni kinyume na mwenendo wa ujirani mwema, bali inakiuka wazi kanuni za kimsingi za sheria za kimataifa na mkataba wa Umoja wa Mataifa, hasa kanuni kuhusu haki ya mamlaka ya kujitawala nchi na kutoingilia masuala ya ndani ya nchi nyingine. Barua ya Mwakilishi wa Kudumu wa Iran katika Umoja wa Mataifa imeendelea kubainisha kuwa: Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa mara nyingine tena inasisistiza kuhusu mamlaka yake isiyoweza kukanushwa kuhusu kumiliki kwake visiwa vya Iran vya Bu Musa, Tomb Kubwa na Tomb Ndogo katika Ghuba ya Uajemi.

Amir Saeid Iravani Balozi na Mwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika Umoja wa Mataifa

 

Jamhuri ya Kiislamu ya Iran pia imelaani vikali matumizi ya jina bandia la Ghuba ya Uajemi katika vifungu vya 11 na 16 vya taarifa iliyotajwa hapo juu na kuiona kuwa ni jambo lisilokubalika. Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imesisitiza kuwa "Ghuba ya Uajemi" ndilo jina pekee la kijiografia halali na lenye itibari la eneo hili la maji.

Jamhuri ya Kiislamu ya Iran daima na katika miaka ya hivi karibuni imekuwa ikitilia mkazo suala la kulindwa kwa hali yoyote mipaka ya nchi kwa lengo la kukabiliana na njama na mipango ya kuzusha mifarakano ya Marekani na waitifaki wake wa Magharibi katika eneo na kuliona hilo kuwa ni katika siasa kuu na isiyobadilika. Jina la Ghuba ya Uajemi linachukuliwa kuwa turathi ya kimaanawi ya ardhi hii, ambayo ina mizizi katika ustaarabu wa Iran na kwa maelfu ya miaka walimwengu wamekuwa wakilitambua eneo hili kwa jina la Ghuba ya Uajemi. Katika hati nyingi za kihistoria na ramani zilizosalia kutoka karne zilizopita, jina la Ghuba ya Uajemi linatajwa, na kulingana na hati za Umoja wa Mataifa, jina la eneo hili ni Ghuba ya Uajemi.

Uingiliaji kati wa wageni umekuwa ni miongoni mwa mambo ambayo yameathiri maamuzi yasiyo sahihi ya baadhi ya nchi katika eneo hili na kuzifanya kuchukua msimamo usio wa kweli na usio sahihi katika suala hili.

Nembo ya Jumuiya ya Nchi za Kiarabu (Arab League)

 

Watafiti ambao wamefanya uchunguzi kuhusiana na  jina la Ghuba ya Uajemi wanakubali kwamba jina lake ni Ghuba ya Uajemi. Jina la Ghuba ya Uajemi limekubaliwa na kuingizwa katika lugha zote zilizo hai za ulimwengu na nchi zote ulimwenguni huita bahari hii Ghuba ya Uajemi.

Katika miaka ya hivi karibuni, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran daima imekuwa ikilipa umuhimu maalumu katika siasa zake za nje suala la kulindwa na kuheshimiwa ardhi yote ya nchi licha ya njama na mipango ya kuuzusha mifarakano ya wageni katika eneo huku ikisisitiza umuhimu wa ujirani mwema na kutangaza utayari wa ushirikiano na majirani zake.

Suala jingine muhimu kwa Iran ni kutilia mkazo juu ya umiliki wa kihistoria na wa milele wa Iran wa visiwa vitatu vya Bu Musa, Tomb Kubwa na Tomb Ndogo.

 

Nyaraka zenye itibari za kimataifa zinathibitisha kuwa, visiwa vitatu vya Bu Musa, Tomb Ndogo na Tomb Kubwa katika Ghuba ya Uajemi ni mali ya Iran. Kwa mfano, ramani ya jeshi la majini la Uingereza mnamo mwaka 1881 inaonyesha ramani ya Wizara ya Masuala ya Bahari ya Uingereza ya mwaka 1863 na pia ramani ya Iran iliyochorwa na Wizara ya Vita ya Uingereza mwaka1886. Katika ramani hiyo, visiwa hivyo vimepakwa rangi ya ardhi ya Iran, na kuna mifano ya hati za kimataifa zinazoonyesha mamlaka ya Iran kwa ya visiwa hivi.

Kwa hakika, malengo ya sera za kigeni za Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni kuzingatia urafiki na ushirikiano na nchi za eneo hili, na bila shaka kutoa madai ya uwongo na yasiyo na msingi hakuna faida nyingine ghairi ya kuandaa uwanja na mazingira ya uingiliaji na hatua za maajinabi katika masuala ya ndani ya eneo hili. Nukta kuu ni kulinda mamlaka ya kujitawala na umoja wa ardhi yote ya nchi, jambo ambalo viongozi wa Iran wamelikokoteza na kutilitia mkazo mara chungu nzima na kulitaja kama mstari mwekundu wa malengo ya kimkakati ya Iran katika eneo.

Tags