Ghalibaf: Baraza la Ushirikiano la Ghuba ya Uajemi lisitekwe na kampeni za vita za Israel
(last modified 2024-10-20T11:07:51+00:00 )
Oct 20, 2024 11:07 UTC
  • Ghalibaf: Baraza la Ushirikiano la Ghuba ya Uajemi lisitekwe na kampeni za vita za Israel

Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge) la Iran amesema kuwa, Baraza la Ushirikiano la Ghuba ya Uajemi linapaswa kuelewa na kutumia vizuri nguvu zake za dhati, lisikubali kutekwa na kampeni za kivita za utawala wa Kizayuni na liache kutoa madai yasiyo na msingi kuhusu ardhi ya Iran.

Kwa mujibu wa shirika la habari la IRNA, Mohammad Bagher Ghalibaf, amesema hayo katika kikao cha wazi cha Bunge leo Jumapili na kusisitiza kuwa, Umoja wa Ulaya na nchi nyingine zinazopenda kupayuka, zinapaswa kutambua kuwa visiwa vitatu vya Bu Musa, Tomb Kubwa na Tomb Ndogo ni sehemu isiyeotenganishika na ardhi ya Iran na hakuna yeyote mwenye uthubutu wa kuchukua hatua dhidi ya uhakika huo wa wazi na wa kihistoria.

Baraza la Ushirikiano la Ghuba ya Uajemi na Umoja wa Ulaya zimeshirikiana katika madai yasiyo na msingi kuhusu visiwa vitatu vya Iran vya Tomb Kubwa, Tomb Ndogo na Bu Musa.

Shahid Yahya Sinwar

 

Spika wa Bunge la Iran pia amesema kuwa, kupanga na kuendelesha operesheni tata na ya kishujaa mno ya Kimbunga cha al Aqsa ni katika kumbukumbu tukufu za shahid Yahya Sinwar za umri wake uliojaa baraka. Operesheni hiyo imebadilisha milingano ya kiusalama, kijeshi na kisiasa katika eneo hili na ni pigo kubwa lisilofidika ulilopata utawala pandikizi wa Kizayuni katika kutoka kwa wanamapabano wa Kiislamu. 

Yahya Sinwar, Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS aliuawa shahidi akiwa mstari wa mbele wa mapambano dhidi ya wanajeshi makatili wa Israel katika mji wa Rafah wa kusini mwa Ukanda wa Ghaza tarehe 16 mwezi huu wa Oktoba 2024.

Tags