Rais Rouhani ahutubia Mkutano wa Kimataifa wa Mabaraza ya Miji na Mameya
Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesiistiza juu ya ulazima wa kuweko ushirikiano wa kimataifa kwa ajili ya kuwa na amani ya kudumu duniani kote.
Akizungumza leo katika Mkutano wa Kwanza wa Kimataifa wa Mabaraza ya Miji na Mameya hapa mjini Tehran, Rais Hassan Rouhani amesema kuwa njia pekee ya kukomesha ghasia, uchupaji mipaka na ugaidi ni kuzidisha uvumilivu, kuheshimiana kiutamaduni kila upande, na jamii mbalimbali kukurubiana zaidi katika masuala ya utamaduni na mitindo ya maisha yao.
Rais Rouhani: Mabaraza ya miji hii leo yanaweza kuwa njia bora ya kusimamia kuendesha na kustawisha miji ya Iran ya Kiislamu.
Rais Rouhani ameongeza kuwa ushirikianao kati ya mabaraza ya miji ya pembe mbalimbali duniani kunaweza kuimarisha zaidi na zaidi mahusiano baina ya jamii, kiutamaduni, kiuchumi, kijamii, kielimu na kiuongozi kati ya mataifa na serikali mbalimbali.
Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran pia amesema kuwa kuanzishwa mabaraza ya miji na vijiji ni hatua yenye umuhimu mkubwa katika njia ya demokrasia ya kidini na Kiislamu ya Iran na kubainisha kuwa hii leo mabaraza ya miji hii leo yanaweza kuwa njia bora ya kusimamia kuendesha na kustawisha miji ya Iran ya Kiislamu kwa upande wa kiikolojia na kiutamaduni na vile vile katika upande wa utamaduni.