Sep 25, 2024 07:56 UTC
  • Tehran yakadhibisha tuhuma za maafisa wa Sweden dhidi ya Iran

Ubalozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Sweden umekadhibisha tuhuma zisizo na msingi na za uongo zilizotolewa na maafisa wa serikali ya Sweden dhidi ya Tehran.

Kwa mujibu wa shirika la habari la IRNA, ubalozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Sweden umetoa taarifa ukipinga tuhuma zinazotolewa na maafisa wa Sweden  dhidi ya Iran kwamba imetuma maelfu ya jumbe fupi kupitia simu za mkononi kwa watu nchini humo ikiwataka kulipiza kisasi kuhusiana na kuchomwa moto nakala za Qur'ani Tukufu hapo mwaka 2023.

Taarifa ya Ubalozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Sweden imeeleza kuwa: Kutolewa na kuchapishwa kwa madai hayo katika vyombo vya habari kunatia sumu na kuathiri anga ya uhusiano wa nchi hizo mbili.

Ubalozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran mjini Stockholm umesema kuwa, vyombo rasmi vya serikali ya Sweden vinatarajiwa kuzuia kutolewa kwa madaikama hayo yasiyo na msingi dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, na katika hali ambayo kwa uamuzi sahihi wa mahakama ya Sweden, wahusika wa kuivunjia heshima Qur’ani Tukufu wamefunguliwa mashitaka, wasiruhusu suala hili kuleta utata na tashwishi.

 Ofisi ya Mwendesha Mashtaka wa Sweden ilitoa madai hayo ya uongo siku ya Jumanne ikisema kwamba, Idara ya Intelijensia ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran mwaka jana ilidukua opereta ya kutuma ujumbe mfupi (SMS) ikiwahimiza watu kulipiza kisasi dhidi ya wale waliohusika na kuchomwa moto nakala za Qur’ani Tukufu nchini Sweden.

Tags