Jul 23, 2016 07:21 UTC
  • Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran, Bahram Qassimi
    Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran, Bahram Qassimi

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amelaani shambulio la kigaidi lililotekelezwa katika mji wa Munich, Ujerumani na kutoa mkono wa pole kwa wananchi na serikali ya nchi hiyo.

Bahram Qassimi amesema kuwa mapambano dhidi ya ugaidi wa aina zote na mahala popote ni takwa la jadi na la dharura la jamii ya kimataifa; na kwamba mapambano haya yanapaswa kuzingatiwa na nchi zote na kufikiwa muafaka kimataifa.  

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesisitiza kuwa leo hii kuuliwa watu wasio na hatia na wasio na ulinzi kumegeuka na kuwa doa jingine katika historia ya mwanadamu, na kwamba  hakuna njia nyingine ya kutokomeza jambo hilo ghairi ya kuendesha mapambano ya dhati,  makubwa na mbali na vigezo vya undumakuwili.  

 

Shambulio la kigaidi Munich 

Baadhi ya mitandao ya kijamii mjini Munich imeripoti kuwa watu karibu 15 waliuawa jana alasiri katika ufyatuaji risasi katika jumba la biashara mjini humo.  

 

Tags