Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran: Ulaya ni kielelezo cha unafiki
(last modified Wed, 30 Oct 2024 08:12:22 GMT )
Oct 30, 2024 08:12 UTC
  • Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran: Ulaya ni kielelezo cha unafiki

Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Iran amesema kuwa, Ulaya ni kielelezo cha unafiki. Abbas Araghchi ameyasema hayo akijibu matamshi ya uingiliaji kati ya Mkuu wa Sera za Kigeni wa Umoja wa Ulaya baada ya kunyongwa kiongozi wa kundi la kigaidi la "Tondar" nchini Iran.

Akijibu matamshi ya Josep Borrel, Sayyid Abbas Araghchi, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, ameandika kwenye mtandao wa kijamii wa X kwamba: "Afisa wa Sera za Kigeni wa Umoja wa Ulaya, napenda kuamini unaposema kwamba maisha na heshima ya binadamu inapaswa kulindwa, lakini tatizo ni kwamba wenzeko huko Ulaya wanaunga mkono bila haya mauaji ya kimbari huko Gaza na mauaji yanayofanyika huko Lebanon.

Araghchi amesema, hivi hauna maoni yoyote kuhusu suala la " Umoja wa Ulaya kuchukua hatua" za kukomesha mauaji ya Wapalestina zaidi ya 50,000 huko Gaza?

Abbas Araghchi pia amehoji kwa nini Umoja wa Ulaya hauchukui hatua za kukomesha wimbi la wakimbizi milioni moja na nusu nchini Lebanon na kuhakikisha kurejea majumbani mwao? 

Vilevile amemuuliza, Umoja wa Ulaya una mpango gani wa kuchukua hatua za kuzihami familia za watu waliouawa na Jamshid Sharmahd? na kumwambia Josep Borrel kwamba: Kama huna jibu, tunapaswa kusema kwamba Ulaya ni kielelezo cha unafiki.

Jamshid Sharmahd

Baada ya miaka mingi ya uovu na jinai za kundi la mamluki na la kigaidi la "Tondar" dhidi ya raia wa Iran ya Kiislamu, "Jamshid Sharmahd", kiongozi wa kundi hilo la kigaidi lililohusika na mauaji ya mamia ya Wairani wasio na hatia ilinyongwa juzi Jumatatu, Oktoba 28, kutokana na uamuzi wa mahakama.

Jamshid Sharmahd

Sharmahd, aliyezaliwa nchini Iran mwaka 1955 ni raia wa Ujerumani na mkazi wa Marekani, na alikuwa kiongozi wa kundi la kigaidi la Tondar linalojulikana nchini Iran kwa kuandaa na kutekeleza mashambulizi mengi ya kigaidi dhidi ya raia, likiwemo lile lililolenga msikiti wa Shiraz mwaka 2008.

Tags