Mtandao wa "Mir" wa Russia waunganishwa na "Shetab" wa Iran
(last modified Mon, 11 Nov 2024 13:04:51 GMT )
Nov 11, 2024 13:04 UTC
  • Mtandao wa

Mtandao wa Mir miamala ya kibenki na kifedha wa Russia hii leo umeunganishwa na mtandao wa benki wa Iran (Shetab) katika hafla iliyohudhuriwa na Gavana wa Benki Kuu ya Iran.

Idara ya Mahusiano ya Umma ya Benki Kuu ya Iran imetangaza kuwa, mtandao wa miamala ya kifedha wa Mir wa Russia leo, Jumatatu, Novemba 21, umeunganishwa na mtandao wa benki wa Iran (Shetab) katika hafla rasmi iliiyohudhuriwa na Gavana wa Benki Kuu na Wakurugenzi Wakuu wa mabenki.

Kwa mujibu wa tangazo hilo, kwa kuunganisha  mfumo wa malipo ya kadi wa Russia, Mir na Shetab ya Iran, kadi za miamala ya kifedha na kibenki za Iran zitaweza kutumika katika mashine za kutoa pesa (ATM) nchini Russia; na kumuwezesha kila mtu kupokea na kutuma pesa kutoka kwenye kadi za benki za Iran kwa njia ya rubles kutoka kwenye ATM za Russia.

Pia, raia wa Russia nchini Iran wanaweza kufaidika na huduma hiyo nchini Iran katika awamu ya pili ya mradi huu, na katika awamu ya tatu, kadi za Shetab za benki za Iran zinaweza kutumika katika maduka nchini Russia.

Makubaliano haya ya Iran na Russia yatazidisha kasi ya kufutwa sarafu ya dola katika miamala ya ya kifedha na kibenki baina ya nchi hizo mbili.dola ya 

Vilevile yatapelekea kudhoofika sarafu hiyo ya Marekani katika miamala ya kimataifa na kuzipa faida nchi zinazojiunga na huduma hiyo.