Baqhaei: Iran haitaki kupoteza muda katika mazungumzo
(last modified Mon, 26 May 2025 10:23:54 GMT )
May 26, 2025 10:23 UTC
  • Baqhaei: Iran haitaki kupoteza muda katika mazungumzo

Msemaji huyo wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema: Tatizo kubwa zaidi katika eneo letu hili litabakia kuwa ni kuendelea mauaji ya umati huko Palestina mauaji ambayo yanaumiza moyo wa kila mtu aliye huru, na huwezi kuzungumzia mambo yanayoendelea katika eneo hili na kunyamazia kimya jinai za utawala wa Kizayuni. Aidha amesema, Iran haitaki kupoteza muda kwenye mazungumzo.

Ismail Baghaei, amesema hayo leo asubuhi katika mkutano wake wa kila wiki na waandishi wa habari. Amesema: "Tulikuwa na matukio kadhaa muhimu wiki iliyopita; Jukwaa la Mazungumzo la Tehran lilikuwa tukio muhimu na lilitoa fursa ya kufikiria na kutafakari juu ya maendeleo ya kieneo na kimataifa, kwa ajili ya amani na usalama wa kimataifa.

Msemaji huyo wa Wizara ya Mambo ya Nje ameendelea kusema: "Tatizo kubwa zaidi katika eneo letu linabakia kuwa ni kuendelea mauaji ya umati yanayofanywa na utawala wa Kizayuni katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu na Wazayuni. Mauaji hayo yanaumiza moyo wa kila mtu aliye huru, na huwezi kuzungumzia matukio ya eneo hili na kunyamaza kimya mbele ya jinai za utawala wa Kizayuni. Leo tu, katika uhalifu wa hivi karibuni zaidi wa Israel dhidi ya skuli moja huko Ghaza, utawala wa Kizayuni umeua shahidi karibu watu 50 wasio na hatia. Mauaji haya ya umati yanaendelea mbele ya kimya cha kutisha cha jamii ya kimataifa na kutochukua hatua Marekani na baadhi ya nchi za Magharibi za kuzuia jinai za Israel."

Akijibu swali kuhusiana na kuondoka mapema mjumbe mkuu wa Marekani wakati wa mazungumzo ya Roma, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema: "Jambo hilo hata si kitu cha kupoteza wakati kukizungumzia. Hiyo ni sehemu ya kujifurahisha vyombo vya habari tu. Kila kitu kwenye mazungumzo kilikuwa wazi, yataanza saa ngapi na yatamalizika saa ngapi na mazungumzo yalianza na kumalizika vizuri kama yalivyopangwa. Baada ya kumalizika mazungumzo tulipaswa kufanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Oman kwa kama dakika 20 hivi, hivyo kilikuwa ni kitu cha kawaida mtu kubakia kwenye mazungumzo hayo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Oman hadi pale muda ulipomruhusu.