Spika Qalibaf: Iran haitakubali makubaliano yoyote bila kuondolewa vikwazo
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza kuwa Iran iko tayari kujenga imani mkabala wa kuondolewa vikwazo huku ikidumisha urutubishaji wa madini ya urani, akieleza kuwa Iran haitakubali makubaliano yoyote pasi na kuondolewa vikwazo ilivyowekewa.
Mohamed Baqir Qalibaf amesema hayo katika ufunguzi wa kikao cha Bunge leo asubuhi, wakati wa kuwaenzi mashahidi wa ugaidi katika Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu. Spika wa Bunge Mohammad Baqir Qalibaf alisema: "Tunajivunia kwamba sisi ni nchi ambayo, kwa kujitolea mhanga kwa Shahidi Qassem Soleimani na mashahidi walinzi wa haram na maeneo matakatifu, iliweza kulisambaratisha kundi la kigaidi la Daesh na kukwamisha njama za Marekani kama alivyokiri Rais wa nchi hiyo kwamba, ndtaifa hilo ndilo lililoanzisha kundi hilo la kigaidi.
Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge la Iran) ameeleza kuwa, pendekezo la Marekani ndani ya fremu ya mazungumzo ya nyuklia halikutaja suala la kuondolewa vikwazo na kusema: Tabia ya Marekani katika mazungumzo ya nyuklia yasiyo ya moja kwa moja inakinzana na haina uaminifu.
Qalibaf amesisitiza kuwa, Marekani haionekana kuna na nia safi na njema katika mazungumzo hayo.
Matamshi ya Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu yanaakisi misimamo rasmi ya Iran katika mazungumzo ya nyuklia na kusisitiza juu ya kulindwa maslahi ya taifa, mamlaka ya kujitawala na muqawama dhidi ya mashinikizo ya kigeni. Matamshi haya pia bila shaka ni ujumbe kwa jamii ya kimataifa na Marekani, yakisisitiza haja ya kubadilishwa utendaji katika mazungumzo ili kufikia makubaliano ya haki.