Kiongozi Muadhamu ateua makamanda wapya kuchukua nafasi ya waliouawa shahidi na Israel
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i127514
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameteua makamanda wapya wakuu wa jeshi kuchukua nafasi ya waliouliwa shahidi na utawala haramu wa Israel
(last modified 2025-06-15T08:05:10+00:00 )
Jun 13, 2025 12:40 UTC
  • Kiongozi Muadhamu ateua makamanda wapya kuchukua nafasi ya waliouawa shahidi na Israel

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameteua makamanda wapya wakuu wa jeshi kuchukua nafasi ya waliouliwa shahidi na utawala haramu wa Israel

Kufuatia mashambulizi ya utawala  Israel, Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Seyyed Ali Khamenei ameteua wakuu wapya wa kijeshi katika nyadhifa kuu, akisisitiza kuendelea nguvu za kiroho ndani ya Vikosi vya Wanajeshi wa Iran.

Uteuzi huo unaashiria upangaji upya wa haraka katika ngazi za juu zaidi za jeshi la Iran katika kukabiliana na matukio mapya ya kijeshi katika eneo hili. Uteuzi huo mpya ni ishara ya azma na irada thabiti ya Iran wakati huu ikijiandaa kukabiliana na tukio lolote katika eneo.

Katika uteuzi huo mpya, Kiongozi Muadhamu amemteua Luteni Jenerali Abdolrahim Mousavi kuwa Mkuu wa Majeshi ya Iran kuziba nafasi ya Meja Jenerali Mohammad Baqeri aliyeuawa aalifajiri ya leo.

Ayatullah Khamenei amesema katika taarifa yake: "Kwa kuzingatia kuuawa shahidi kwa kifahari Luteni Jenerali Mohammad Hossein Bagheri mikononi mwa utawala wa Kizayuni uliolaaniwa, na kwa kuzingatia utumishi wako wa kupongezwa na uzoefu wako muhimu, ninakuteua kuwa mkuu mpya wa majeshi ya Iran.Aidha katika uteuzi mwingine, Kiongozi Muadhamu ambaye ni amirijeshi mkuu wa majeshi ya Iran amemteua Luteni Jenerali Ali Shadmani kuwa kamanda wa makao makuu ya Kikosi cha Khatam al-Anbiya, akichukua nafasi ya Meja Jenerali Gholam Ali Rashid,aliyeuawa shahidi pia leo katika mashambulio ya leo ya Israel dhidi ya Iran.

Wakati huo huo, Ayatullah Khamenei amemteua Luteni Jenerali Mohammad Pakpour kuwa mkuu mpya wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH akichukua nafasi ya kamanda shujaa aliyeuawa shahidi leo pia Luteni Jenerali Hussein Salami.