Iran iko tayari kwa ajili ya uchaguzi
(last modified Sun, 21 Feb 2016 02:46:55 GMT )
Feb 21, 2016 02:46 UTC
  • Iran iko tayari kwa ajili ya uchaguzi

Waziri wa Mambo ya Ndani Iran amesema mipango ya imekamilika kwa ajili ya uchaguzi wa Bunge na Baraza la Wataalamu wiki hii.

Ali Ridha Rahmai Fadhli akinzungumza katika mahojiano na Kanali ya Kwanza ya Televisheni ya Iran Jumamosi usiku amesema, masanduku 129,000 ya kupigia yamewekwa katika vituo 53 vya kupigia kura kote Iran. Aidha amesema zaidi ya maafisa nusu milioni watasimamia zoezi la uchaguzi mwaka huu.

Rahmani-Fadhli amesema hadi sasa hakua ukiukwaji wa sheria ulioripotiwa katika kampeni ambazo zitamalizika Alhamisi tarehe 25 Februari, siku moja kabla ya uchaguzi. Ammeongeza kuwa usalama umeimarishwa na kwamba kuna maafisa wa kutosha wa usalama watakaokuwa na jukumu la kulinda masanduku ya kupigia kura. Amesema kuwa wawakilishi wa wagombea na vyama wataruhusiwa kuwa katika maeneo ya kupigia na kuhesabia kura.

Wairani milioni 54, wametimisha masharti ya kupiga kura katika uchaguzi ujao wa mwezi huu wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran na Baraza la Wanazuoni Wataalamu Wanaomchagua Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu.

Tags