Rais Rouhani: Ulimwengu wa Kiislamu utakombolewa kwa misimamo ya wastani
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i16972-rais_rouhani_ulimwengu_wa_kiislamu_utakombolewa_kwa_misimamo_ya_wastani
Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema, Ulimwengu wa Kiislamu utakombolewa tu kwa misimamo ya wastani na kupambana na utumiaji mabavu.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Oct 08, 2016 03:36 UTC
  • Rais Rouhani: Ulimwengu wa Kiislamu utakombolewa kwa misimamo ya wastani

Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema, Ulimwengu wa Kiislamu utakombolewa tu kwa misimamo ya wastani na kupambana na utumiaji mabavu.

Rais Rouhani ameyasema hayo mapema leo asubuhi katika mji wa Kuala Lumpur Malaysia alipokutana na   wasomi wa ngazi za juu na wakuu wa vyombo vya habari katika nchi hiyo.

Katika hotuba yao, rais wa Iran ametoa wito wa kuwepo umoja wa Waislamu na jitihada zakuinua hadhi na nguvu za Ulimwengu wa Kiislamu. Rais Rouhani amesema Ulimwengu wa Kiislamu unahitaji umoja, usalama na ustawi. Ametaka mambo yanayotishia mustakabali wa Ulimwengu wa Kiislamu kuwa ni pamoja na  misimamo mikali ya kidini, ukosefu wa matumaini na kukosekana hisia ya kujiamini.

Rais Rouhani amebainisha misingi muhimu ya sera za Iran katika eneo la Magharibi mwa Asia na kusema: "Kupambana na magaidi wakufurishaji katika medani ya vita, kusaidia katika kupatikana amani, usitishaji vita na kuwafikishia misaada ya kibinadamu waathirika wa vita, kuzuia kugawanywa vipande vipande nchi za eneo na kuheshimiwa kura za wananchi katika kuchagua serikali."

Rais Rouhani amesema madola ya Magharibi bado yanakusudia kuendeleza sera zao za kibeberu na kuongeza kuwa, si tu kuwa madola ya maghairbi yanakusudia kueneza  ubeberu katika sekta za sayansi na teknolojia bali pia yanalenga kuendeleza ukoloni wa kiutamaduni.

Rais wa Iran amesema wasomi na wanafikra wa Ulimwengu wa Kiislamu wana jukumu muhimu katika kipindi hiki cha historia.