Rais Rouhani: Uchaguzi ni miongoni mwa mambo ya kujivunia Iran
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i1822-rais_rouhani_uchaguzi_ni_miongoni_mwa_mambo_ya_kujivunia_iran
Rais Hassan Rouhani amesema uchaguzi ni miongoni mwa mambo ya kujivunia kwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Feb 24, 2016 00:09 UTC
  • Rais Rouhani: Uchaguzi ni miongoni mwa mambo ya kujivunia Iran

Rais Hassan Rouhani amesema uchaguzi ni miongoni mwa mambo ya kujivunia kwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Akizungumza katika kikao cha Baraza Kuu la Mapinduzi ya Kiutamaduni la Iran, Rais Rouhani ametaja sifa na utukufu wa Bibi Fatimatuz Zahra (AS) na jinsi maisha ya mtukufu huyo yalivyo na mafunzo katika maisha na kusisitiza kuwa: adhama ya ujudi na uwepo wenye taathira wa bibi Fatima katika nyuga mbalimbali za kisiasa na kijamii unaonyesha kuwa propaganda hasi dhidi ya dini ya Mwenyezi Mungu kuhusiana na mtazamo wake juu ya wanawake, ni madai batili na yasiyo na msingi.

Rais Rouhani amebainisha kuwa wanakosea wale wanaofikiri kwamba uhuru na maendeleo ya wanawake yanapatikana kwenye utamaduni na fikra za Kimagharibi.

Akiashiria kuhusu uchaguzi utakaofanyika tarehe 26 mwezi huu wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu, yaani Bunge la Iran pamoja na wa Baraza la Wanazuoni Wataalamu wanaomchagua Kiongozi Mkuu, Rais Rouhani amesema moja ya sababu zinazoifanya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran iendelee na harakati yake kwa ukakamavu na uwezo mkubwa licha ya matatizo na kila aina ya njama dhidi yake, ni mhimili imara wa wananchi na uendeshaji nchi kulingana na irada ya wananchi hao unaofanyika kupitia uchaguzi.../