Rais Rouhani asisitiza kuarifishwa uwezo wa Iran katika nchi zingine duniani
Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza kuhusu ulazima wa kuarifishwa uwezo wa Iran kwa ajili ya wawekezaji wa sekta binafsi kutoka nchi zingine duniani.
Rais Rouhani ameyasema hayo leo mjini Tehran alipokutana na mabalozi wapya wa Iran katika nchi za Nambibia, Qatar, Norway, Macedonia, Ghana, Serbia na Bulgaria. Amewataka mabalozi hao kuhakikisha kuwa uhusiano wa Iran na nchi hizo unaimarishwa.
Wakati huo huo Rais Hassan Rouhani leo amekutana na mabalozi wapya wa nchi kadhaa za kigeni ambao wanawakishal nchi zao hapa Iran. Kati ya mabalozi wapya wa nchi za kigeni ambao Rais Rouhani amewapokea ni mabalozi wapya wa Sierra Leone, Sweden na Uingereza na pia mabalozi wasio wakaazi wa Albania, Colombia na Moldova. Katika mazungumzo yake na balozi mpya wa Uingereza nchini Iran, Nicholas Hopton, Rais Rouhani amesistiza kuhusu ulazima wa pande mbili katika mapatano ya nyuklia kutekeleza ahadi zao.
Hali kadhalika katika mkutano wake na balozi mpya wa Sierra Leone nchini Iran, Almamy Camara, Rais Rouhani amesema Iran inataka kuimarisha uhusiano wa kiuchumi na kiutamaduni na Sierra Leone. Kwa upande wake Camara amesema nchi yake inakaribisha mashirika ya Iran kuwekeza nchini humo. Aidha amesema nchi yake inajitambua kama mshirika wa Iran katika masuala ya kimataifa hasa katika vita dhidi ya ugaidi.