Iran: Madola makubwa yasivuruge mapatano ya nyuklia
(last modified Fri, 18 Nov 2016 04:23:19 GMT )
Nov 18, 2016 04:23 UTC
  • Reza Najafi
    Reza Najafi

Balozi wa Iran katika Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki IAEA amesema madola sita makubwa duniani ya kundi la 5+1 hayapaswi kuchukua hatua za kuvuruga utekelezaji mapatano ya nyuklia baina yao na Tehran.

Reza Najafi ameyasema hayo Alhamisi na kuongeza kuwa, Iran inaendelea kutekeleza ahadi zake katika mapatano ya nyuklia yajulikanayo kama Mpango Kamili wa Utekelezaji (JCPOA) baina yake na madola sita makubwa duniani. Aidha amesema Iran inachunguza kwa karibu kuona iwapo  madola yote husika yanatekeleza mapatano hayo.

Tarehe 16 Januari mwaka huu, Iran na nchi tano wanachama wa kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ambazo ni Russia, China, Ufaransa, Uingereza na Marekani pamoja na Ujerumaini, zilianza utekelezaji wa makubaliano ya nyuklia maarufu kwa jina la JCPOA ambayo yalitiwa saini tarehe 14 Julai, 2015. Mazungumzo kuhusu mapatano hayo yalisimamiwa na Umoja wa Ulaya.

Wahusika wakuu katika Mapatano ya Nyuklia baina ya Iran na 5+1

Kwa mujibu wa makubaliano hayo, Iran ilikubali kuwekea mipaka fulani miradi yake ya nyuklia na upande wa pili nao ukaahidi kuondoa vikwazo vyote vya kidhulma ilivyowekewa Iran kutokana na miradi yake ya nyuklia yenye malengo ya amani.

 

Tags