Zarif: Iran inafanya juhudi za kuimarisha muqawama wa taifa la Palestina
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i21316-zarif_iran_inafanya_juhudi_za_kuimarisha_muqawama_wa_taifa_la_palestina
Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, taifa hili daima limekuwa likifanya juhudi za kuimarisha safu za muqawama, mapambano na mshikamano wa taifa la Palestina.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Dec 12, 2016 23:20 UTC
  • Zarif: Iran inafanya juhudi za kuimarisha muqawama wa taifa la Palestina

Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, taifa hili daima limekuwa likifanya juhudi za kuimarisha safu za muqawama, mapambano na mshikamano wa taifa la Palestina.

Dakta muhammad Javad Zarif alisema hayo jana katika mazungumzo yake hapa mjini Tehran na Ramadhan Abdullah Shallah, Katibu Mkuu wa Harakati ya Jihadul Islami ya Palestina ambapo sambamba na kutangaza bayana himaya na uungaji mkono usiotetereka wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa malengo matukufu ya Palestina amesema kuwa, katika ulimwengu huu mpya hakuna nchi au nguvu ambayo inaweza kufanya mambo peke yake na kusonga mbele.

Dakta Zarif amesema kuwa, utawala wa Kizayuni wa Israel uwe peke yake au kwa kusaidiwa na baadhi ya madola yenye nguvu duniani hauwwezi kufikia katika malengo yake.

Dakta Zarif, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran

Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza kwamba, Iran itaendelea kuliunga mkono taifa madhulumu la Palestina katika juhudi zake za kupigania ukombozi na kukabiliana na jinai za utawala haramu wa Israel.

Katika mazungumzo hayo, Ramadhan Abdullah Shallah, Katibu Mkuu wa Jihadul Islami alimpatia ripoti Dakta Zarif kuhusiana na hali ya sasa ya Palestina, makundi ya Kipalestina, uvamizi unaoendelea wa utawala vamizi wa Israel na kuendelea ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni.