Rais Rouhani: Iran inakaribisha kustawisha uhusiano na Umoja wa Ulaya
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i22537-rais_rouhani_iran_inakaribisha_kustawisha_uhusiano_na_umoja_wa_ulaya
Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, Iran inakaribisha kwa mikono miwili ushirikiano katika nyuga zote na Umoja wa Ulaya ikiwemo nchi ya Romania.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Dec 31, 2016 23:34 UTC
  • Rais Rouhani: Iran inakaribisha kustawisha uhusiano na Umoja wa Ulaya

Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, Iran inakaribisha kwa mikono miwili ushirikiano katika nyuga zote na Umoja wa Ulaya ikiwemo nchi ya Romania.

Rais Rouhani amesema hayo leo baada ya kupokea hati ya utambulisho ya balozi mpya wa Romania hapa mjini Tehran na kubainisha kwamba, Iran na Romania zina mambo mengi ambayo kupitia kwayo zinaweza kuimarisha ushirikiano, hivyo kuna haja ya kutumiwa fursa hizo.

Rais Rouhani ameashiria mipango mikubwa ya Iran yenye lengo la kustawisha njia za mawasiliano hususan usafiri na uchukizi wa reli na kuongeza kuwa, Romania inaweza kuwa mlango wa Iran kwa ajili ya kuingia Ulaya kupitia njia ya Bahari Nyeusi na vilevile Romania nayo inaweza kuingia katika soko la Asia na Mashariki ya Kati kupitia Iran.

Michael Klor-Berchtold, balozi mpya wa Ujerumani mjini Tehran akikabidhi hati ya utambulisho kwa Rais Hassan Rouhani

Kwa upande wake, Adrian Kozjacski, balozi mpya wa Romania mjini Tehran amesisitiza katika mazungumzo yake na Rais Rouhani kwamba, Bucharest imeazimia kukuza ushirikiano wake na Tehran katika nyanja zote ambazo pande husika zina hamu ya kustawisha uhusiano wao.

Aidha Rais Rouhani amesema katika mazungumzo yake na balozi mpya wa Ujerumani hapa mjini Tehran kwamba, Ujerumani ni mshirika wa kwanza wa kibiashara wa Iran barani Ulaya na kusisitiza juu ya kuimarisha ushirikiano wa nchi hizo katika nyanja mbalimbali.

Rais Rouhani amezungumzia makubaliano ya nyuklia kati ya Iran na madola sita makubwa duniani na kusisitiza juu ya kutekelezwa kikamilifu makubaliano hayo.