Rouhani: Iran inapinga jaribio lolote la kuzigawa nchi za Mashariki ya Kati
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i22648-rouhani_iran_inapinga_jaribio_lolote_la_kuzigawa_nchi_za_mashariki_ya_kati
Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa hii leo nchi nyingi zimekiri na kukubali mchango na nafasi yenye taathira kubwa ya Jamhuri ya Kiislamu katika kuimarisha amani na utulivu kwenye eneo la Mashariki ya Kati na kwamba, Iran imekwamisha njama za kutaka kuzigawa nchi za ene hilo.
(last modified 2026-02-21T22:51:18+00:00 )
Jan 02, 2017 03:46 UTC
  • Rouhani: Iran inapinga jaribio lolote la kuzigawa nchi za Mashariki ya Kati

Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa hii leo nchi nyingi zimekiri na kukubali mchango na nafasi yenye taathira kubwa ya Jamhuri ya Kiislamu katika kuimarisha amani na utulivu kwenye eneo la Mashariki ya Kati na kwamba, Iran imekwamisha njama za kutaka kuzigawa nchi za ene hilo.

Rais Rouhani ambaye jana usiku alikuwa akihojiwa na Kanali ya Pili ya Televisheni ya Taifa amesema kuwa, lengo kuu la kwanza la Jamhuri ya Kiislamu ni kuimarisha usalama na utulivu katika Mashariki ya Kati na kwamba nchi za eneo hili haziwezi kupata maendeleo na ustawi bila ya kuwa na usalama na amani.

Rais Rouhani amesema vita vya ndani na mashambulizi ya nchi moja dhidi ya nyingine ni hatari kubwa na kwamba ugaidi ni hatari kwa Mashariki ya Kati na dunia nzima. Amesisitiza kuwa, kupambana na ugaidi ni lengo la pili kuu la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na kusema Tehran iko tayari kuisaidia nchi yoyote ile katika kupambana na ugaidi.

Rais Hassan Rouhani akihojiwa na waandishi habari

Rais wa Jamhuri Kiislamu ya Iran amepinga jaribio lolote la kutaka kubadilisha mipaka ya kijiografia ya nchi za Mashariki ya Kati na kusema: Baadhi ya madola yalitaka kuzigawa nchi za Syria, Iraq na Yemen lakini Iran imepinga suala hilo na inasisitiza suala la kusimama kidete, kupambana na juhudi za kidiplomasia kwa ajili ya kupata ufumbuzi wa  masuala mbalimbali.

Ameashiria shambulizi la kigaidi lililolenga sherehe za mwaka mpya mjini Istanbul huko Uturuki na kusema: Kuua wanadamu wasio na ulinzi ni suala linalopaswa kulaani na kwamba shambulizi hilo limeonesha tena kuwa ugaidi hauna huruma kwa yeyote na iwapo hazitafanyika jitihada za kweli za kukabiliana nao basi kirusi hicho kitawasibu wanadamu wote.