Iran kuitupa sarafu ya dola baada ya maamuzi ya kibaguzi ya Trump
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i24533-iran_kuitupa_sarafu_ya_dola_baada_ya_maamuzi_ya_kibaguzi_ya_trump
Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imesema inapanga kuacha kutumia sarafu ya dola katika taarifa rasmi za kifedha kufuatia hatua ya wakuu wa Washington kuiweka nchi hii katika orodha ya nchi saba ambazo raia wake wanazuiwa kuingia Marekani.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Feb 01, 2017 00:51 UTC
  • Iran kuitupa sarafu ya dola baada ya maamuzi ya kibaguzi ya Trump

Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imesema inapanga kuacha kutumia sarafu ya dola katika taarifa rasmi za kifedha kufuatia hatua ya wakuu wa Washington kuiweka nchi hii katika orodha ya nchi saba ambazo raia wake wanazuiwa kuingia Marekani.

Gavana wa Benki Kuu ya Iran Valiullah Seif amenukuliwa na vyombo vya habari akisema Iran itaitupa dola na kuanza kutumia sarafu mpya ya kigeni au kapu la sarafu kadhaa katika taarifa shughuli na taarifa zake zinazohusu fedha za kigeni.

Seif amesema hatua hiyo itaanza kutekelezwa Machi 21, 2017 wakati wa kuanza mwaka mpya wa Hijria Shamsia ambao pia huwa mwanzo wa mwaka mpya wa kifedha nchini.

Rais Trump wa Marekani

Iran ilikuwa na mpango huo  wa kutupa sarafu ya dola ya Marekani lakini uamuzi huo umepatiwa kasi zaidi baada ya rais Donald Trump kutia saini sheria ya kuwapiga marufuku raia kutoka nchi saba za Kiislamu kuingia nchini  humo. Nchi ambazo zimelengwa na sheria hiyo ni pamoja na Iran, Iraq, Syria, Yemen, Libya, Sudan na Somalia.

Hatua hiyo imelaaniwa vikali na Iran ambayo imesema itachukua hatua kadhaa kukabiliana na uhasama huo wa Marekani.