Mamilioni washiriki maandamano ya kuadhimisha ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu hapa Iran
(last modified Fri, 10 Feb 2017 08:18:04 GMT )
Feb 10, 2017 08:18 UTC
  • Mamilioni washiriki maandamano ya kuadhimisha ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu hapa Iran

Mamilioni ya wananchi wa matabaka mbali mbali wa Iran wanashiriki maandamano ya amani katika kila pembe ya nchi, kuadhimisha sherehe za miaka 38 ya Ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu nchi hapa.

Hapa mjini Tehran, Wairani wa matabaka yote, wanaume kwa wanawake, wazee kwa vijana, licha ya baridi kali wamejumuika katika Medani ya Azadi, ambapo waliwasili kupitia barabara 10 zilizoainishwa na serikali.

Hadi tunaenda mitamboni, Rais Hassan Rouhani wa Iran alikuwa analihutubia taifa katika Medani ya Azadi hapa Tehran.

Sehemu ya Wairani wanaosherehekea ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu

Mbali na Tehran, sherehe hizi za kuadhimisha miaka 38 ya Ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu zinafanyika katika miji 1000 na vijiji 4000 kote nchini. Kadhalika maadhimisho haya ya kihitioria yanafuatiliwa kwa karibu na waandishi wa habari zaidi ya 6000 wa ndani na nje ya nchi.

Mbali na kubeba bendera ya Iran na mabango yenye picha za Muasisi wa Mapinduzi wa Kiislamu, Imam Khomeini MA na Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Khamenei, waandamanaji hao wamebeba mabango na maberamu yenye jumbe za kuilaani Marekani na hususan utawala mpya wa Rais Donald Trump wenye chuki dhidi ya Uislamu na Waislamu. 

Rais Rouhani na maafisa wengine wa ngazi za juu serikalini

Itakumbukwa kuwa, katika siku kama hii ya leo miaka 38 iliyopita, Iran ilikuwa katika siku ya kihistoria itakayokumbukwa siku zote, ambapo wananchi wanamapinduzi wa taifa hili walihitimisha kipindi cha giza totoro katika historia ya Iran kwa kuung'oa madarakani utawala wa kidikteta wa Shah Pahlavi, uliokuwa ukiungwa mkono na madola ya Magharibi haswa Marekani.

Tags