Brigedia Dahqan: Misaada ya Iran, sababu ya kusindwa maadui
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i26094-brigedia_dahqan_misaada_ya_iran_sababu_ya_kusindwa_maadui
Waziri wa Ulinzi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa Iran ya Kiislamui daima inayaunga mkono na kuyasaidia makundi ya mapambano na kwamba uungaji mkono huo umewalazimisha maadui kurudi nyuma na kushindwa.
(last modified 2026-02-21T22:51:18+00:00 )
Mar 08, 2017 04:26 UTC
  • Brigedia Dahqan: Misaada ya Iran, sababu ya kusindwa maadui

Waziri wa Ulinzi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa Iran ya Kiislamui daima inayaunga mkono na kuyasaidia makundi ya mapambano na kwamba uungaji mkono huo umewalazimisha maadui kurudi nyuma na kushindwa.

Brigedia Jenerali Hussein Dahqan amesema kuwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni mfumo wa kisiasa unaojitawala na haitasimama au kuondoka katika njia hiyo.

Kuhusu uwezo wa kujihami wa Iran Dahqan amesema uwezo huo unadhamini usalama wa taifa mbele ya vitisho vya adui. Amesema ujumbe wa Mapinduzi ya Kiislamu umewafikia walimwengu na kuwa na taathira kubwa.

Waziri wa Ulinzi wa Iran

Ameashiria njama zinazofanywa na madola ya kibeberu kwa ajili ya kuwa na ushawishi na kupenya katika eneo la Mashariki ya Kati na ulimwengu kwa ujumla na kusema kuwa, watawala wasiokuwa na nafasi madhubuti ya kijamii kati ya mataifa yao wa Mashariki ya Kati ndio wanaotayarisha njia ya kuwepo madola na majeshi ya nchi za kigeni katika eneo hili.