Marekani imefeli katika njama za chuki dhidi ya Iran
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i27530-marekani_imefeli_katika_njama_za_chuki_dhidi_ya_iran
Njama za kila namna za Marekani katika kueneza chuki dhidi ya Iran zimefeli na hazijaweza kubadilisha fikra za waliowengi nchini humo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Apr 09, 2017 23:09 UTC
  • Marekani imefeli katika njama za chuki dhidi ya Iran

Njama za kila namna za Marekani katika kueneza chuki dhidi ya Iran zimefeli na hazijaweza kubadilisha fikra za waliowengi nchini humo.

Uchunguzi mpya wa maoni uliofanywa na shirika la IBD la Marekani umebaini kuwa, Wamarekani wengi hawajahadaiwa na propaganda za serikali ya nchi yao kuwa eti Iran ni tishio kwa usalama wa dunia. Uchunguzi huo wa maoni umebaini kuwa ni asilimia tano tu ya Wamarekani ndio wanaoiamini serikali yao inapodai kuwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni tishio kwa usalama wa taifa la Marekani.

Aghalabu ya raia wa Marekani wanaamini kuwa makundi ya kigaidi kama vile ISIS na Al Qaeda ndio tishio kubwa kwa usalama wao. Walioshiriki katika uchunguzi huo wa maoni walisema Russia na Korea Kaskazini kwa taratibu ndio tishio kwa usalama wa taifa la Marekani.

Timu ya mieleka ya Marekani ikiwasili Iran, Februari 2017

Uchunguzi huo unakuja baada ya uchunguzi mwingine wa hivi karibuni wa Chuo Kikuu cha Pennsylvania cha Marekani kubaini kuwa aghalabu ya wasomi duniani wanakiri kuhusu uwezo mkubwa wa kijeshi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Aidha kwa mujibu wa tathmini ya kila mwaka ya Mashirika ya Kijasusi ya Marekani, vitisho vya kiintaneti kuanzia mwaka 2011 vimechukua nafasi ya ugaidi kama tishio la kwanza kwa usalama wa taifa la Marekani. Ugaidi umeibuka tena kama tishio nambari moja kutokana na hujuma kadhaa za kigaidi katika nchi za Ulaya ambazo ni natija ya sera zisizo sahihi za nchi hizo katika kuunga mkono Marekani na utawala wa Israel.