Kiongozi Muadhamu atoa dola 85,000 ili kuachiliwa wafungwa walio na madeni
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ametoa kiasi cha dola 85,000 kwa lengo la kusaidia kuachiliwa huru wafungwa wenye makosa yasiyo ya kukusudia ikiwa ni katika kulipa fidia ya makosa yao.
Ayatullah Ali Khamenei alitoa kiasi hicho cha fedha Jumapili iliyopita ambacho kimepelekwa kwa kitengo cha dia cha Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa lengo la kuachiliwa huru wafungwa wa makosa yasiyo ya kukusudia. Kwa mujibu wa habari hiyo jumla ya wafungwa 7500 watanufaika na misaada kama hiyo ya kifedha ambayo inakusanywa kutoka kwa wananchi na viongozi wa mihimili mitatu ya dola nchini hapa.
Rais Hassan Rouhani wa Iran ametoa karibu dola 72,000 huku Ali Larijani, Spika wa Bunge na Ayatullah Sadeq Larijani, Mkuu wa Vyombo vya Mahkama kila mmoja akitoa kiasi cha dola 3000. Sherehe za kuachiliwa huru wafungwa wa makosa yasiyo ya kukusudia ambazo zitasimamiwa na kitengo cha dia cha Iran, zitafanyika jioni ya Jumanne ya leo mjini Tehran.