Iran yataka mashindano ya silaha Mashariki ya Kati yakomeshwe
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i31022-iran_yataka_mashindano_ya_silaha_mashariki_ya_kati_yakomeshwe
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Mohammad Javad Zarif amesema kuna haja ya kuwepo jukwaa la kustawisha mazungumzo baina ya nchi za Ghuba ya Uajemi huku akitoa wito kwa nchi za eneo hili kukomesha mashindano yao ya silaha.
(last modified 2026-09-18T11:23:09+00:00 )
Jun 27, 2017 03:21 UTC
  • Iran yataka mashindano ya silaha Mashariki ya Kati yakomeshwe

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Mohammad Javad Zarif amesema kuna haja ya kuwepo jukwaa la kustawisha mazungumzo baina ya nchi za Ghuba ya Uajemi huku akitoa wito kwa nchi za eneo hili kukomesha mashindano yao ya silaha.

Akizungumza mjini Berlin Ujerumani Jumatatu katika Baraza la Sera za Kigeni la Ulaya, Zarif amesema mashindano ya silaha Mashariki ya Kati yanatokana na uhusiano wa nchi za Magharibi na baadhi ya nchi za eneo.

Aidha Zarif ametoa wito kwa nchi za Ulaya kutumia ushawishi wao kupungua mzozo katika Ghuba ya Uajemi ambao umeibuka baada ya Saudi Arabia kuchochea waitifaki wake kukata uhusiano na nchi jirani ya Qatar.

Emir wa Qatar Sheikh Tamim Aal Thani

Saudi Arabia, Bahrain, Misri na Umoja wa Falme za Kiarabu zimekata uhusiano wa kidiplomasia na Qatar na pia kuiwekea nchi hiyo mzingiro wa nchi kavu, angani na baharini. Nchi hizo zimedai kuwa Qatar inaunga mkono ugaidi na kuvuruga uthabiti katika eneo madai ambayo wakuu wa Doha wameyakanusha.  Zarif amesema nchi hizo ambazo zinaituhumu Qatar kuunga mkono ugaidi pia zimetoa tuhuma hizo zisizo na msingi dhidi ya Iran lengo likiwa ni kufunika kufeli kwao katika kukidhi mahitaji ya watu wao.