Iran kamwe haitalegeza msimamo mbele ya Marekani na maadui wengine
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i31206-iran_kamwe_haitalegeza_msimamo_mbele_ya_marekani_na_maadui_wengine
Waziri wa Ulinzi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza kuwa, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kamwe haitalegeza msimamo mbele ya maadui na kwamba nchi hii itatoa jibu kali kwa vitisho vyovyote vile.
(last modified 2026-04-19T09:26:01+00:00 )
Jul 01, 2017 09:03 UTC
  • Iran kamwe haitalegeza msimamo mbele ya Marekani na maadui wengine

Waziri wa Ulinzi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza kuwa, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kamwe haitalegeza msimamo mbele ya maadui na kwamba nchi hii itatoa jibu kali kwa vitisho vyovyote vile.

Brigedia Jenerali Hussein Deqhan ameyasema hayo Jumamosi na kuongeza kuwa mafanikio makubwa ya kijeshi Iran ni natija ya jitihada za wasomi na wataalamu Wairani. Ameogneza kuwa, Marekani katu hautoweza kuizuia Iran kustawi.

Waziri wa Ulinzi wa Iran ameashiria mpango wa vikwazo vipya vya Marekani dhidi ya Iran na kusema, Iran imeshajiainishia njia itakayo katika shughuli zake za kuunda makombora na kujihami.

Brigedia Jenerali Dehqan amesema nguvu na uwezo wa Iran umetokana na mfumo uliokita mizizi na imara wa Jamhuri ya Kiislamu na kuongeza kuwa, taifa la Iran haliogopi hata kidogo vikwazo vya Marekani.

Kombora la Balistiki la Emad likifanyiwa majaribio nchini Iran

Tarehe 15 Juni Baraza la Senate la Marekani lilipasisha muswada wenye uhasama wa kuendeleza vikwazo dhidi ya Iran katika sekta za makombora na silaha nyinginezo. Marekani inadai kuwa etu majaribio ya makombora ya Iran ni kinyume cha azimio 2231 la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. Pamoja na hayo Alceo Smerilli msemaji Federica Mogherini Mkuu wa Sera za Kigeni wa Umoja wa Ulaya amekiri kuwa majaribio ya makombora ya Iran hayakuiki sheria za kimataifa.

Iran inasisitiza kuwa azimio 2231 linazuia tu kuundwa makombora yenye kusheheni vichwa vya nyuklia katika hali ambayo nchi hii haiundi makombora kama hayo wala  haimiliki zana za nyuklia. Kwa mujibu wa Fatwa ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran, utumizi wa silaha za nyuklia ni haramu.