Nchi zilizostawi zashindana kuja kuwekeza nchini Iran
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i3211
Ayatullah Akbar Hashemi Rafsanjani, Mkuu wa Halmashauri ya Kuainisha Maslahi ya Mfumo wa Kiislamu wa Iran amesema kuwa, nchi zilizoendelea zinashindana kwa ajili ya uwekezaji hapa nchini.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Mar 17, 2016 01:50 UTC
  • Nchi zilizostawi zashindana kuja kuwekeza nchini Iran

Ayatullah Akbar Hashemi Rafsanjani, Mkuu wa Halmashauri ya Kuainisha Maslahi ya Mfumo wa Kiislamu wa Iran amesema kuwa, nchi zilizoendelea zinashindana kwa ajili ya uwekezaji hapa nchini.

Ayatullah Rafsanjani amesema kuwa, ushindani wa nchi zilizoendelea na mashirika muhimu ya kimataifa kwa ajili ya kuja kufanya uwekezaji hapa nchini unatokana na nafasi ya Iran katika jamii ya kimataifa na kwamba, fursa na uwanja wa kufanya mambo makubwa umeandaliwa nchini Iran. Mkuu wa Halmashauri ya Kuainisha Maslahi ya Mfumo wa Kiislamu wa Iran aidha amebainisha kuwa, nchini Iran wananchi ndio wanaochukua maamuzi na kwamba, taifa hili ni mfano wa kuigwa wa nchi za Mashariki ya Kati na hata kwa nchini nyingi duniani katika uwanja huu.

Ikumbwe kuwa, baada ya Iran na madola sita makubwa duniani kufikia makubaliano ya nyuklia mwaka ulipoita na baadaye kufuatiwa na kuondolewa vikwazo vya kidhulma ilivyokuwa imewekewa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, viongozi wa nchi na mashirika mbalimbali wamekuwa wakifanya safari hapa nchini kwa shabaha ya kutafuta uwezekano wa kuwa na ushirikiano na taifa hili katika nyanja mbalimbali hususan za kibiashara.