Dakta Velayati: Siasa za Uholanzi na Marekani kuhusu JCPOA zinatofautiana
(last modified Sun, 22 Oct 2017 14:00:10 GMT )
Oct 22, 2017 14:00 UTC
  • Dakta Velayati: Siasa za Uholanzi na Marekani kuhusu JCPOA zinatofautiana

Mshauri wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu katika masuala ya kimataifa amesema katika mazungumzo yake hapa mjini Tehran na ujumbe wa kibunge wa Uholanzi kwamba, siasa za Uholanzi na Marekani kuhusiana na makubaliano ya nyuklia ya JCPOA zinatofautiana.

Dakta Ali Akbar Velayati amesema hayo katika mazungumzo yake hapa mjini Tehran na Raymond Knops Kaimu Mkuu wa Kamisheni ya Mahusiano ya Kigeni ya Bunge la Ulaya pamoja na ujumbe alioandamana nao na kusisitiza kwamba, hatua ya Uholanzi ya kuunga mkono makubaliano ya nyuklia yanayojulikana kwa jina la Mpango Kamili wa Pamoja wa Utekelezaji JCPOA imeifanya nchi hiyo iwe mkosoaji wa siasa za Marekani.

Mshauri wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu katika masuala ya kimataifa amewaambia waandishi wa habari baada ya mazungumzo yake hayo kwamba, siasa za Ulaya ikiwemo Uholanzi zinatofautaiana na siasa za Marekani kuhusiana na suala la miradi ya nyuklia ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Abbas Araqchi, Mkuu wa Timu ya Iran katika mazungumzo ya nyuklia

Dakta Velayati ameongeza kusema kuwa, siasa za Ulaya katu hazikubaliani na ukiukaji ahadi wa Marekani, bali madola hayo ya Ulaya yanafungamana kikamilifu na makubaliano ya nyuklia ya JCPOA yaliyofikiwa kati ya Iran na kundi la 5+1 linaloundwa na nchi za Russia, China, Marekani, Ufaransa, Uingereza pamoja na Ujerumani.

Velayati amesema pia kuwa, uhusiano wa Iran na Uholanzi uko katika hatua ya kukua na kwamba, nchi hiyo ya bara Ulaya ina hamu na shauku ya kukuza uhusiano wake wa kibiashara na kiuchumi na Jamhuri ya Kiislamu.

Tags