Spika wa Bunge la Iran kuelekea Pakistan leo
Dakta Ali Larijani, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran leo anatarajiwa kuuongoza ujumbe wa Kibunge wa Iran kuelekea Pakistan kwa ajili ya kushiriki katika mkutano wa kujadili namna ya kukabiliana na ugaidi.
Katika safari yake hiyo ya siku tatu, Dakta Larijani anatarajiwa kuhutubia mkutano uliopewa jina la "Changamoto za Kukabiliana na Ugaidfi na Nafasi ya Ushirikiano wa Kieneo".
Kadhalika Dakta Ali Larijani, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran leo anatarajiwa kukutana na kufanya mazuungumzo pambizoni mwa mkutano huo ana Maspika wa Bunge wa nchi zinazoshiriki katika mkutano huo.
Mkutano wa "Changamoto za Kukabiliana na Ugaidfi na Nafasi ya Ushirikiano wa Kieneo" unafanyika kwa ubunifu wa Bunge la Taifa la Pakistan.
Taarifa zaidi zinasema kuwa, mkutano huo unatarajiwa kuanza kesho Jumapili na utahudhuriwa na Maspika wa Bunge kutoka nchi sita za Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Russia, Afghanistan, Uturuki, China na mwenyeji Pakistan.
Ajenda kuu ya mkutano huo ni kujadili namna ya kukabiliana na changamoto zilizoko katika vita dhidi ya ugaidi na kuandaa mikakati ya ushirikiano wa kieneo katika uwanja huo.
Tatizo la ugaidi na harakati za makundi ya kigaidi ni tatizo kuu la ulimwengu kwa sasa, na nchi mbalimbali zimekuwa zikifanya jitihada za kuwa na ushirikiano wa kieneo na kimataifa katika vita dhidi ya ugaidi.