Iran kati ya nchi bora katika teknolojia ya Nano duniani
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i3802-iran_kati_ya_nchi_bora_katika_teknolojia_ya_nano_duniani
Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni kati ya nchi 10 bora duniani katika teknolojia ya Nano.
(last modified 2025-11-04T03:09:21+00:00 )
Mar 26, 2016 01:41 UTC
  • Iran kati ya nchi bora katika teknolojia ya Nano duniani

Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni kati ya nchi 10 bora duniani katika teknolojia ya Nano.

Hayo yamesemwa na Saeed Sarkar, Mkuu wa Idara ya Ustawi wa Teknolojia ya Nano katika Kitengo cha Sayansi cha Ofisi ya Rais wa Iran.

Ameongeza kuwa, Iran hivi sasa inashindana na madola makubwa duniani kama vile Japan, Ujerumani na Korea Kusini katika uga wa teknolojia ya Nano. Amesema hivi sasa baada ya kufikiwa mapatano ya nyuklia na kuondolewa vikwazo, nchi nyingi zinataka kushirikiana na Iran katika uga wa Nano. Amesema hadi sasa Russia, Thailand, China na nchi kadhaa za Amerika ya Latini zimetia saini makubaliano na Iran katika uga wa teknolojia ya Nano.

Nano ni teknolojia mpya inayohusu matumizi ya vitu vidogo sana na miundo yake ambayo inapimwa kuwa kati ya nanomita 1-100.

Asili ya Nano ni nanomita ambayo ni kipimo cha sehemu ya bilioni moja ya mita. Hii inamaanisha vitu ambavyo ni vikubwa kuliko atomi na vidogo mara 1000 kuliko upana wa unywele.