Russia: Iran haijakiuka maazimio ya kimataifa
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia amesema kuwa nchi yake inapinga hatua yoyote ya kuweka vikwazo dhidi ya Iran kwa sababu Tehran haijakiuka azimio lolote kwa kufanya majaribio ya makombora.
Gennady Gatilov amesema Russia haikubaliana na hatua yoyote ya kuiwekea vikwazo Iran na kwamba suala hilo halipaswi hata kujadiliwa kwa kutumia kisingizio kwamba Tehran imefanya majaribio ya makombora.
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia amesema Moscow imelieleza waziwazi la Usalama la Umoja wa Mataifa msimamo wake wa kupinga vikwazo dhidi ya Iran na kuongeza kuwa, Iran haijakiuka azimio lolote la Baraza la Usalama.
Gennady Gatilov amesema kuwa hakuna sheria yoyote inayoizuia Iran kufanya majaribio ya makombora.
Siku chache zilizopita Marekani na baadhi ya nchi za Magharibi zilikosoa majaribio ya makombora yaliyofanywa na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa kutumia vijisababu visingizio mbalimbali.